SEHEMU YA TATU

TABIA MAADILI NA ADABU ZA KIISLAAM

Uislaam unasisitiza sana na kutilia mkazo na hima kubwa juu ya tabia za kibinadamu  na inatili umuhimu sana adabu za kijamii, mpaka ilifikia Mtume (s.a.w) akalifanya lengo la kutumwa kwake ni kutimiza maadili na tabia zilizo njema na kuyatawanya kwa watu wote pale alipo sema :

1. إنما بعثت لأ تمم مكارم الأخلاق

(Hakika si jambo jingine nimetumwa ili kukamilisha maadili mema).

Na Mwenyezi Mungu anapo taka kumsifia Mtume wake na kipenzi chake (s.a.w) anamsifia kwa sifa ya maadili mema na mazuri na anasema:

2. وإنّك لعلى خلق عظيم

(Hakika wewe ni mwenye tabia  (maadili) njema na ya hali ya juu.

Na wakati anapo taka kuukumbusha umma wa kiisalaam rehma waliyo zawadiwa, anawakumbusha kwa kutaja alama kubwa ya rehma hiyo nayo si nyingione bali ni: ulaini wa tabia yake (s.a.w) na anasema:

3. فبما رحمة من الله لنت لهم

Kutokana na rahma kutoka kwa Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao.

Pamoja na dalili hizi na zinginezo ambazo ni nyingi sana katika maudhui haya, zinazo julisha juu ya umuhimu wa maadili na tabia na adabu katika Uislaam na upeo wa Uislaam katika kuhimiza nakuonyesha namna unavyotaka kuthibiti kwa vitu hivi kwa Muislaam, hata  Qur’ani tukufu inapo taja baadhi ya hukumu zinazo husiana na adhabu  huzifuatisha kwa kutaja msamaha na kufuatia kueleza upande wa kimaadili na tabia na kuusifu msamaha katika adhabu hizo kuwa uko karibu  zaidi na ucha Mungu.

 

 NGUZO ZA  MAADILI TABIA NA ADABU

 Ndio, hakika  Uislaam umeifanya dini na ucha Mungu kuwa ndio vigezo vya madili na tabia na ukaitambulisha tabia (maadili) kwa kutaja nguzo nne na kwa ajili ya adabu ukataja nguzo mbili na kuwahimiza Waislaam kujipamba nazo na kuwaamrisha kujipamba na maadili hayo.

 

NGUZO NNE ZA MAADILI

Ama nguzo nne za maadili (tabia) ni kama zifuatazo:

1- Utwahara wa moyo na ukweli wa Nia, Mwenyezi Mungu amesema kuhusiana na umuhimu wa utwahara wa moyo na usalama wake (usafi wake) na kuhusiana na ukweli wa Nia na usafi wke:

4. يوم لا ينفع مال ولا بنون, إلّا من أتي الله بقلب سليم

(Siku ambayo haitamfaa mtu mali wala watoto, isipokuwa atakae mwendea Menyezi Mungu kwa Moyo safi).1 Atakae mwendea Mwenyezio Mungu na moyo ulio safi kutokana na shirki na kufru na ulio safika kutokana na tabia mbaya.

2-Ukunjufu wa uso na kuwa na bashasha, imepokelewa katika Hadithi kama ifuatavyo:                                     

المؤمن بشره في وجهه و حزنه في قلبه

(Muumini furaha yake iko (huonekana) usoni mwake na Huzuni yake huwa Moyoni mwake) na katika Hadithi nyingine:

إن المؤمن هش بش

(Hakika Muumini ni laini  mwenye furaha na mwenye bashasha) na pia imepokelewa:

 إن حسن البشر يكسب المحبة ويد خل الجنة  (Hakika uzuri wa bashasha ni kuwa huleta mapenzi na humuingiza mtu peponi) na:

(عبوس الوجه يبعد من الله ويد خل النار)

  (Kukunja uso humuweka mtu mbali na Mwenyezi Mungu na humuingiza motoni).

3-Kuzungumza vema na kuwa na kauli njema (nzuri), Mwenyezi Mungu mtukufu amesema: [5] وقولوا للناس حسنا (Na wambieni watu yaliyo mema au zungumzeni na watu kwa njia njema).2 Na Amirul Muuminiin (a.s) amesema: [6]إني أكره لكم ان تكونوا سبابين (Hakika mimi ninachukizwa sana kwenu kuwa ni watu wenye kutukana (kulaani)3

4-Kuwa na muamala mzuri na maingiliano mema na watu, Mwenyezi Mungu amesema:

 [7]خذ العفو وأمر بالعرف و أعرض عن الجاهلين (Toa msamaha (wasamehe watu) na uamrishe mema na jiepushe na wajinga). 4 Na amesema Mwenyezi Mungu alie takasika: [8](وإذا خاطبهم الجاهلون قالوا سلا ما) (Na pindi wanapo zungumziwa na majahili (yaani wanapo semewa maneno mabaya) husema amani iwe kwenu kwa maana hawajibizani nao kwa maneno mabaya).

 

NGUZO MBILI ZA ADABU

Ama nguzo za adabu ni mbili kama zifuatazo:

 1-Adabu zinazo mhusu mtu mmoja na hizi ni adabu ambazo zinahusiana na maisha ya mtu binafsi yeye na shakhsia yake, kwa mfano adabu za kula na kunywa, kula na kuamka, nguo ya kuva na sehemu ya kuishi, kusafiri na kuto safiri, swiha (afya) na maradhi, na zinginezo ambazo zimeletwa na Uislaam tena adabu zilizo bora kabisa,  nakusema  kwamba kuzitekeleza humfanya mtu awe karibu na kila jambo la kheri na zuri na kumuweka mbali au kumuepusha na kila lililo la shari na lenye kuchukiza na zinamfanya awe ni mtu mwema na mwenye saada.

2- Adabu za kijamii nazo ni: Adabu ambazo zinahusiana na maisha ya mtu kama jamii (si kama mtu binafsi), kwa mfano adabu za maingiliano na namna ya kutendeana (Muamala) na wazazi wawili, mke,  watoto na jamaa wa karibu na wanafamilia, jirani marafiki, mwanafunzi na mwalimu, na watu wengine wote, bali na vitu vyote vilivyopo ulimwenguni, na katika upande huu Uislaam umetuletea mafundisho yaliyo bora kabisa na adabu zilizo bora, adabu ambazo zinatoa dhamana kwa kuzitekeleza kwake kuwa jamii nilazima itakuwa na amani na usalama,utulivu na uimara wa kijamii na maelewano, kufahamiana, mapenzi na uwiano na maingiliano mazuri kati ya watu wote na kati ya mtu mmoja mmoja kati ya wana jamii.

 

VIPAMBANUZI VYA JAMII YA KIISALAAM

Kisha ni kuwa jamii ya kiislaam ni jamii ambayo hufuata maadili na tabia za kibinadamu na adabu za kijamii ambazo zimeletwa na Dini ya kiislaam, kwa maana hiyo jamii ya kiislaam inatofautiana na jamii nyingine kwa mambo yafuatayo:

1-Jamii ya kiislaam inakuwa na rangi au mfumo mwingine tofauti na jamii hii ambayo tunaishuhudia katika zama zetu hizi, kwani baada ya kuwa ni jamii yenye imani ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, hupambika na maadili na adabu za kiislaam na kwa kufanya hivyo mienendo ya jamii ya kiislam inabadilika na kuboreka ubadilikaji ambao mifumo yote iliyopo ardhini haiwezi kuifikia, na kwa maana hiyo jamii inaenewa na maana kamili ya hali ya kibinadamu ya hali ya juu, wakati ambapo ulimwengu wa leo unampatia mwanadamu umbo la chombo cha kufanyia kazi na kumjaalia au kumfanya kama chuma na kumnyang’anya au kumvua maana zote na hali zote za wema na kheri, kisha utakuta katika jamii ya kiislaam hunatoweka na kufichika yale matatizo ya kinafsi na matatizo mengi tuyashuhudiayo katika zama hizi, kama ambavyo huipatia jamii matumaini na maelewano, na kuenea mapenzi na kupendana na kuhurumiana kati ya mtu na mtu na kati ya jamii na mtu mmoja wote kwa pamoja.

2-Maisha-na pande zake zote-yanakuwa ni maisha yenye kupendeza na kuvutia chini ya kivuli cha nidhamu ya kiislaam iliyo adilifu, na wakati huo miji huimarishwa majumba kujengwa na ardhi kutumika kwa kilimo na viwanda kuendeleea na kupanuka kwa biashara  na mali kuongezeka na watu kuwa matajiri katika anga ambalo hakuna dhulma ndani yake wala jeuri, utumiaji wa nguvu, wala uteroristi, vikwazo, kufungwa pingu, kufungwa jela, kuadhibiwa na matatizo mengineyo na wala hakuwi na ufukara, kwa hivyo ndio maana ujenzi wa miji, maendeleo ya haraka, mapenzi na kuamiana, kuwa na matumaini wakati wa kuutekeleza Uislaam linakuwa ni jambo la kawaida ambalo ulimwengu na walimwengu hawakulishuhudia katika zama hizi hata kama kutakuwa na nyenzo nyingi na zilizo endelea.

3-Kila mtu kati ya watu wa jamii ya kiislaam anakuwa ni mwenye kueneza Uislaam na mafindisho yake kwa kauli yake na matendo yake, na anakuwa ni mwenye kumlinda kila mtu kati ya watu wa jamii yake na watu wa umma wake na anakuwa ni mwenye majukumu juu yao, ana amrisha mema na kukataza mabaya, analingania kwenye Uislaam na katika kuitii serikali na utawala mmoja wa kiisalaam wa kiulimwengu kwa hekima na mawaidha mazuri (Nasaha) na kufanya majadiliano kwa ajili ya kuithibitisha serikali hiyo kwa majadiliano yaliyo mema (au kwa mfumo ulio mzuri).

 

UISLAAM NA MAADILI NI MAPACHA WAWILI

Hakika uhakika wa Uislaam na ukweli wa Dini ya Kislaam, ni: Maadili ya kibinadamu na adabu za kijamii zilizo thabiti na za hali ya juu, hakika vitu viwili hivi ni mapacha wawili ambao kamwe hawaachani wala kutengana, bali wao ni kitu kimoja chenye maana moja, kwani hakuna kitu hata kimoja kilicho bakia na kwenda kinyume kati ya vitu vilivyo himizwa na maadili kati ya vitu vilivyo amrishwa na Uislaam  na hakuna kitu kilicho kwenda kinyume kati ya vitu vilivyo himizwa na kusisitizwa na  Adabu kati ya vitu vilivyo himizwa na kusisitizwa na  Uislaam, kwa hivyo hukumu zote za kiisalaam na mafundisho yake ya hali ya juu, kati ya Ibada na na hukumu za ufanya kazi au muamala  na nyinginezo, zimejengwa juu ya msingi wa maadili ya hali ya juu na kanuni za kiadabu zilizo madhubuti, na kwa ajili ya kuyafafanua hayo tuna ashiria hapa kwa ufupi baadhi ya mambo yaliyo amrishwa na Uislaam kati ya mambo ya wajibu  na kuyakataza mengine kati ya mambo ya haramu na kutoa tahadhari kutokana na mambo hayo kati ya maadili mabaya, na badala yake kuhimiza kutekeleza mambo ya fadhila na adabu, ili tuweze kuona ya kuwa ni kwa namna gani mambo yote hayo yanawiana na maumbile ya mwanadamu na yana nasibiana na roho yake na hali yake ya kimaanawia bali yana wiana na kunasibiana na mwili wake na mambo yake ya kimadda na kwa mustawa wa hali ya juu kabisa wa kimaadili na kiwango cha juu kabisa cha adabu zilizo bora za kibinadamu na za hali ya juu. 

 

MAMBO YA WAJIBU

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

إنّ الله يأ مر بالعد ل والإحسان وإيتاء ذي القربي[9]

(Hakika Mwenyezi Mungu ana amrisha kufanya uadilifu na wema na kuwapa watu wa karibu haki yao) 1 kwa hivyo ni lazima juu ya Muislaam kujifunza mambo ya wajibu na kuyatekeleza, na sisi hapa tutajaribu kutaja kiasi kitakacho tuwia chepesi kukitaja kati ya mambo hayo ya wajibu: 1-Kutoa malipo ya mke na mahali yake. 2-Kutoa malipo ya mnyonyeshaji. 3-Kulipa haki ya uvunaji. 4-Kuwapa watu wa karibu haki zao. 5-Kutoa Zaka. 6-Kutoa au kulipa mali ya mayatima. 7-Kuchukua tahadhari. 8-Kujipamba wakati wa kwenda misikitini (kuvaa vizuri).

9-Kufuata aliyo kuja nayo Mtume(s.a.w) na Ahlul bayti wake (a.s).

10- Kutekeleza au kulipa amana.

11-Kutoa ushahidi. 12-Kutekeleza na kulipa haki za watu na haki za Mwenyezi Mungu. 13-Kuomba ruhusa ya kuingia majumbani.

14-Kuamrisha mema. 15-Kufuata mema yanapo amrishwa.

16-Kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. 17-Kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa dua na maombi. 18-Kujitenga na maadui wa Mwenyezi Mungu na pia maadui wa mawaliii wa Mwenyezi Mungu.

19-Kuwachukia maadui wa Mwenyezi Mungu. 20-Kuwa na wasila wa kukufikisha kwa Mwenyezi Mungu.

21-Kufuata fadhila za Mwenyezi Mungu. 22-Kuwatia tahayari watu wenye kuzua bidaa (uzushi). 23-Kulala kwa mke. 24-Kumfuata Mtume (s.a.w) na Aali zake walio maasumiini (a.s). 25-Kumfuata Imam katika sala. 26-Kuharibu madda au kitu kisababishacho ufisadi. 27-Kutubia.

28-Kusimama kidete juu ya haki na kuto teteleka. 29-Kusimama kidete kwenye jihadi na kuto teteleka. 30-Kujiepusha na dhanna mbaya.

 31-Kujiepusha na ibada ya asie kuwa Mwenyezi Mungu.

32-Kujiepusha na uzuzi, uongo, nyimbo na miziki. 33-kumili na kuelekea kwenye Amani na sulhu. 34-Kumuitikia Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w). 35-Kumpenda Mwenyezi Mungu na kuwapenda mawalii wake. 36-Mwanamke kuvaa hijab kwa wanamume wazio mahramu zake. 37-Kuhijji. 38-Kusimulia neema za Mwenyezi Mungu. 39-Kuharamisha yaliyo haramishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. 40-Kuwana na dhanna nzuri na Mwenyezi Mungu.

41-Kulea watoto. 42-Kuhifadhi tupu (sehemu za siri). 43-Kutekeleza sala na ibada wakati wote bila kukoma, Ahadi, na Amana. 44-Kuhukumu kwa mujibu wa aliyo telemsha Mwenyezi Mungu. 45-Kumtaka mtu alie dhulumiwa kuhalalisha alicho dhulumiwa. 46-Kutoa maamkizi (kutoa salam). 47-Kuwa na moyo wenye unyenyekevu na kumuogopa Mwenyezi Mungu. 48-Kuwaheshimu na kuwaonea huruma wazazi wawili.

49- Kutoa khumsi. 50-Kuwa na khofu ya Mwenyezi mungu (kumuogopa).

51-Kumuomba Mwenyezi Mungu. 52-Kulingania kwenye njia ya Mwenyezi Mungu. 53-Kuitetea dini na nafsi. 54-Kuondoa maovu. 55Kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wote. 56-Kutoa malezi kwa watoto. 57-Kujibu salam na barua. 58-Kuwaongoza watu kwnye haki. 59-Kuridhia kadhaa na maamuzi ya Mwenyezi Mungu. 60-Kumzuru Mtume na maimamu watokanao na kizazi cha Ahlul bayti (a.s).

61-Kusalimu amri na kumsabbihi (kumtakasa) Mwenyezi Mungu. 62- Kuharakia kwenye msamaha wa Mwenyezi Mungu. 63-Kusikiliza Qur’ani tukufu. 64-Kutembea ardhini kwa ajili ya kufanya mazingatio na Ibrah. 65-Kumshukuru Mwenyezi Mungu na wazazi wawili. 66-Kuwa na Subira (uvumilivu). 67-Kuwatendea mema wazazi wawili na jamaa wa karibu. 68-Kuwa mkweli katika mazungumzo. 69-Kusuluhisha kati ya watu. 70-Kufunga Mwezi wa Ramadhani.

71-Mukallaf  kuchukua dhamana ya kitu alicho sababisha uharibifu wake. 72-Kuwalisha wenye njaa. 73-Kutafuta Rizki. 74-Kutafuta elimu. 75-Kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Ulul Amri (wenye mamlaka) (a.s). 76-Kudhihirisha na kubainisha haki. 77-Kudhihirisha kuchukizwa na watu wafanyao maasi. 78-Kumuabudu Mwenyezi Mungu. 79-Kuchukua mazingatio kutoka kwenye vitu vyenye kutia Ibrah. 80- Kufanya uadilifu.

81-Kuishi na mke kwa wema. 82-Kujifunza elimu za wajibu kama Usulud-dini (misingi ya dini) na matawi ya dini (Furuud-dini) na maadili na adabu. 83-Kusaidiana. 84-Kufumba macho na kuto angalia mambo ya haramu. 85-Kuomba istighfari (msamaha kwa Mwenyezi Mungu). 86- Kuwa na ghera (wivu). 87-Kukaa kwa ukunjufu katika vikao. 88- Kusoma elimu ya fiqhi (elimu ya sheria ya dini). 89-Kuzifikiria Neema za Mwnyezio Mungu na alama zake.90-Kuhukumu kwa haki.

91-Kusimamisha dini na Kutekeleza amri zake. 92-Kuwa na kauli njema. 93-Kuwa na msimamo katika mambo. 94-Kufanya kazi ya halali. 95-Kuwa pamoja na wakweli. 96-Kuzuwia kulaaniwa kwa Mwenyezi Mungu. 97-Kuwazuwia makafiri kuingia misikitini. 98-Kujutia madhambi uliyo yafanya. 99-Kumnasihi Muumini na kumnusuru. 100- Kutoa pesa katika njia ya Mwenyezi Mungu.

101- Kuoa (kufanya nikah). 102-Kukataza maovu. 103-Kujizuwia kufanya mambo yaliyo katazwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. 104-Kurejea kwa Mwenyezi Mungu. 105-Kuwa na nia njema na ya kweli. 106-Kusali sala za Tahajjud (sala za Usiku). 107-Kuhama. 108-Kuharibu mambo ya upotovu. 109-Kuwapenda watu wa karibu ya Mtume (Ahlul bayti wake). 110-Kujikinga na mambo yaliyo haramishwa na Mwenyezi Mungu.

111-Kupima kwa kipimo kilicho safi na kilicho nyooka. 112- Kuteleleza Ahadi. 113-Kuikinga nafsi na ahli zako kutokana na moto. 114-Kutawakkali kwa Mwenyezi Mungu katika mambo mbali mbali. 115-Kuwa na yakina na Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho.

 

 

MAMBO YA HARAMU

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

قل تعالوا أتل ما حرم ربكم عليكم[10]

(Sema njooni nikusomeeni aliyo yaharamisha mola wenu juu yenu). Kwa hakika kama ambavyo ni lazima kwa Muislaam kujifunza mambo ya wajibu na kuyatekeleza, vilevile ni lazima kujifunza  mambo ya haramu na kujiepusha nayo, na sisi tunajaribu hapa kutaja mambo ya haramu yaliyo mengi na ambayo ndiyo ambayo hukumbana nayo katika maisha yetu ya kila siku:

1-Kutoa usaidizi katika kufanyika kwa Maasi. 2-Kumsaidia dhalimu. 3-Kujiaminisha na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. 4-Kupinga Muujiza. 5-Kupinga kiama na ufufuo wa kiwiliwili au asili moja wapo kati ya Usulud-dini na misingi ya madhehebu.6-Kupinga jambo moja wapo kati ya mambo ya dharura katika dini. 7-Kujiepusha na utajo wa Mwenyezi Mungu. 8-Kuwacheza shele na kuwafanyia istihzaa waumini. 9-Kufanya israafu (matumizi mabaya). 10-Kufanya madhambi madogo mara kwa mara bila kuacha.

11-Mwanamume kuvaa pete ya dhahabu. 12-Kupiga Punyeto.: yaani kutoa manii kwa mkono au bila kutumia mkono. Ndio, inajuzu kupiga punyeto kupitia kwa mke. 13-Kuwaudhi waumini. 14-Kujiepusha na hukumu za kisheria. 15-Kutumian chombo cha Dhahabu na Fedha hata kama ni kwa ajili ya mapambo. 16-Kuwadhalilisha Waislaam na kuwadharau. 17-Kufichua siri ambayo mwenye nayo haridhiki wala kufurahia. 18-Kufichua siri ya kila mmoja kati ya mke na mume.19-Mke kuto mtii mumewe katika mambo ambayo ni wajibu kwake kumtii. 20- Watoto kuto watii wazazi wawili.

21-Kucheza Kamari kwa kuweka badala (Hii ni aina ya uchezaji wa kamari ulio maarufu katika nchi ya Iraq ambapo hutumia pete kwa kuificha mikononi na upande wa pili kuchagua mkono wenye pete na kujipatia pesa au kitu kilicho wekwa ikiwa atapatia). 22-Kukiri kufanya maasi. 23-Kueneza maovu. 24-Kula katika Mwezi wa Ramadhani au katika funga maalum ya wajibu bila udhuru wa kisheria. 25-Kuficha chakula akisubiri kupanda kwa bei. 26-Kuto jikinga na mkojo au najisi zingine. 27-Kumpinga Mwenyezi Mungu katika uamuzi wake na makadirio yake (Qadha na Qadar yake).28-Kuamrisha maovu. 29- Kumuudhi jirani. 30-Kuchukua malipo juu ya mambo ya wajibul ainiyyah (yaliyo lazima kuyatekeleza kwa kila mtu yeye mwenyewe) katika sura ya ujumla.

31-Kumnyenyekea na kumtii dhalimu. 32-Kuitia nafsi kwenye hatari na maangamio. 33-Kumnasibisha mtoto kwa mtu mwingine asie kuwa baba yake. 34-Mwanamke kutoka nyumbani bila ya idhini ya mumewe. 35-Mwanamume na mwanamke kila mmoja kumbusu mtu mwingine asie kuwa mahram. 36-Mwanamume kumbusu mwanamume mwenzie kwa matamanio sawa awe ni mwanamume au mwanamke isipokuwa mume na mkewe na walii na mjane na mwenye kuhalalishiwa kweke na mhalalishwa. 37-Kuzua bidaa katika dini. 38-Kufunga ndoa mwanamume na mwanamke ambae ni haramu kwake kumuoa.

39-Kuwadhania watu vibaya au kuwa na dhanna mbaya na watu pamoja na kufuatisha athari kwenye dhanna hiyo. 40-Kuzua mambo au uongo.

41-Kujisaidia haja hali ya kuwa umekielekea au umekipa mgongo kibala. 42-Kutakabari kunako kumuabudu Mwenyezi Mungu. 43- Mwanamume kujipamba kwa dhahabu. 44-Kupiga ramli vyovyote iwavyo. 45-Kuwa na kiburi au Kutakabburi. 46-Kuacha sala za wajibu. 47-Kuacha wajibu wowote kati ya mambo mengine ya wajibu. 48- Kuchelewesha ibada ya hijja kunako mwaka wa kupata uwezo. 49- Kupinga na kukadhibisha jambo lolote lililomo kwenye Qur’ani au hukumu za kisheria. 50-Kuacha kuvaa Ihraam.

51-Kutumia kwa fujo (kupita kiasi). 52-Kuto Sali sala katika wakati wake hadi muda wake ukamalizika. 53-Kupeleka mashtaka kwa dhalimu bila ya kuwepo ulazima au dharura ya kufanya hivyo. 54-Kuhudhuria kwenya mambo ya kipuuzi. 55-Mwanamke kujipamba kwa jili ya mwanmume wa nje (yaani sie mumewe). 56-Kumtumikisha malaika au roho au majini na vinginevyo. 57-Kumlewesha mtu kwa madawa kuliko enea siku hizi. 58- Kufanya ghushi (udanganyifu) na kugeuza mambo vyovyote itakavyo kuwa kwa sura ya ujumla. 59-Kuchelewesha kulipa funga ya Ramadhani hadi mwenzi mwingine wa Ramadhani. 60-Kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu.

61-Kuacha kuwaadabisha watoto jambo ambalo hupelekea kuharibika kwao na kuwa mafasidi. 62-Kuharamisha jambo la halali, na kuhalalisha jambo la haramu. 63-Kufanya ujasusi katika aibu za watu. 64-Kumtia khofu Muumini. 65-Kuacha kufanya takiya katika sehemu za dharura. 66- Kujifananisha na Makafiri katika mavazi au kujipamba kicha na mengineyo. 67-Kumjeruhi yeyote au kumpiga na kumtukana au kukata kiungo moja wapo kati ya viungo vyake. 68-Kuto itikia salam. 69- Kuhukumu kwa sheria zizo telemshwa na Mwenyezi Mungu mtukufu.70- Kuzuia haki za Mwenyezi Mungu.

71-Kuzuia haki za watu. 72-Kumfunga mtu kwa uonevu. 73- Mwanamume kuvaa Hariri bila ya kuwepo udhuru wa kisheria. 74- Kufanya husuda na kufuatisha athari juu ya husuda hiyo. 75-Kupoteza haki za watu.76-Kuhifadhi na kuweka vitabu vya upotevu na majarida magazeti na makala yenye kupotosha watu na kuyauza au kuyanunua na kujifunza vitabu hivyo na kuwafundisha watu na kuyaeneza pia kuvisambaza vitu hivyo. 77-Kula mali ya mayatima. 78-Kunywa vileo (mvinyo). 79-Kula mzoga. 80-Kula nyama ya nguruwe.

81-Kula nyama ya mnyama ambae ni haramu kuliwa. 82-Kula nyama ya mnyama ambae hakuchinjwa kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu mtukufu au kwa kuto timiza sharti moja wapo kati ya masharti ya kuchinja. 83-Kula odongo au vitu vingine vya haramu. 84-Kufanya khiyana. 85-Kuuza, kununua, kuhifadhi na kuvitumia vyombo vya lahau na miziki. 86-Kufanya hadaa na udanganyifu. 87-Kumchumbia mwanamke mwenye mume au ambae yuko kwenye eda. 88-Kula mbegu mbili za mbuzi (Mapumbu). 89-Kula vitu vingine vilivyo haram katika mnyama alie chinjwa. 90-Kuuza mbwa mgomvi na nguruwe na kuwanunua.

91-Kutoka na kuasi amri ya Imam wa kisheria na muadilifu. 92-Kula na kunywa najisi na kitu kilicho najisika. 93-Kumsemea uongo Mwenyezi Mungu, Mtume na Imam (a.s). 94-Kupiga dufu na kupuliza zumari na mfano wa hayo. 95-Kuiba. 96-Kueneza mambo ya batili. 97-Kuficha na kuififiza haki.

MAMBO MENGINEYO YA HARAMU

1-Kuridhia mkeo kutembea na wanaume wengine na kuto kuwa na wivu na kuwaunganisha watu kwa ajili ya kufanya maasi ya kijinsia. 2-Kusema uongo. 3-Kujiunga na vyama vya kisiasa vya batili kama vyama vya kikomonisti na mfano wa hivyo. 4-Kuingia na kujiunga na dini za upotovu kama madhehebu za kisufi na madhehebu ya babiy na mfano wa hayo. 5-Kumfanyia Uadui Mumini. 6-Kuwapenda maadui wa dini au kuwa na urafiki nao bila ya kuwa na dharura ya kufanya hivyo. 7-Kutukana moja kwa moja hasa kumtukana Mwenyezi Mungu alie takasika na Mtume (s.a.w) na maimam na kuitukana dini, Kitabu, Madhehebu, na mambo mengine matukufu katika dini au madhehebu. 8-Kugusa maandishi ya Qur’ani bila ya twahara. 9-Mtu kuwa na ndimi mbili yaani (kuwa ndumila kuwili) unapokuwepo hukusifia na ukighibu na kuondoka kulamba kisogo na kukusema. 10-Kupokea na kuchukua rushwa na kutoa rushwa kwa ajili ya kuficha ukweli na kudhihirisha batili.

11- Kupokea na kutoa rushwa katika mambo ya serikali isipokuwa kwa dharura. 12-Kupokea na kutoa Riba na kuitolea ushahidi kwa maandishi na kuwa kiunganishi cha uchukuaji au utoaji wa riba. 13- Kubakia katika chi ambayo mtu hawezi kuhifadhi na kubakia kwenye utekelezaji mambo ya dini na kutekeleza amri za dini yake ya kiisalaam. 14-Kwenda kwenye nchi ambazo kufanya hivyo kutasababisha madhara kwa mtu kuhusiana na dini yake. 15-Kuiba kwa kuvizia njiani.

16-Kunyoa ndevu au kuzirefusha kwa mashine zenye kulainisha. 17- Kunyoa ndevu za mtu mwingine. 18-Kucheza miziki. 19-Kushiriki katika mashindano ya mavazi. 20- Kwenda kwenye shule ambazo ni sababu ya mtu kuharibika na kuingia kwnye ufisadi.

21- Kwenda kwenye Mabafu au mahodhi ya kuogelea na kwenye mashule na mikutano au mijumuiko ambayo kuna mchanganyiko kati ya wanamume na wanawake. 22-Kuto itika wito na kutekeleza amri za kisheria za Mwenyezi Mungu, Mtume, Ahlul bayti na maraajiu (viongozi wa juu wa kidini) katika mambo wayatoleayo hukumu. 23-Kuridhia maasi. 24-Kumtuhumu mtu kwa uzinifu. 25-Kueneza maneno kati ya watu kwa lengo ya kutia ufisadi au sharri. 26-kuyasikiliza. 27- Kuhudhuria kwenye sinema za ufisadi.  28-Kujishughulisha na uharibifu wa misikiti. 29-Kufanya kazi na kwenda kwa madhalimu. 30- Kutengeneza vyombo vya lahau (upuuzi) na kamari msalaba na mfano wa hivyo.

31- Kuimba na kulia kwa maombolezo kwa kusema maneno ya batili. 32-Kuziba barabara ya Waislaam. 33-Kumuaibisha Muumini na kumdharau na kumtukana. 34-Kudharau madhambi na kuyaona ni madogo jambo ambalo hupelekea kuchelewesha tawbah. 35-Wanawake kutoka hovyo na kutoka bila kujisitiri wala kuvaa hijab. 36-Kumshirikisha Mwenyezi Mungu mtukufu. 37-Kueneza uovu. 38-Kupinga kiapo au kukataa kuapa. 39-Kwenda kinyume na  ahadi (makubaliano). 40-Kutoa ushahidi wa uongo.

41-Kuwekeana sharti na rehani isipokuwa katika mambo yaliyo tajwa katika kitabu cha mashindano na kulenga shabaha. 42-Kufanya mazingaombwe. 43-Kufanya unafiki. 44-Kuwakubalia udhuru madhalimu na watu wa bidaa wazuao mambo na kuwafanya marafiki. 45-Mtu kupoteza na kuto mjali mtu ambae anasimamia mambo yake. 46- Kucheza na njiwa na ndege na mfano wa hayo, mambo ambayo hupelekea mtu kufanya mambo ya haramu. 47-Kudhulumu na kufanya uadui kwa watu wengine. 48-Al-dhihaar (mwanamume kumwambia mkewe ya kuwa wewe ni kama mgongo wa mama yangu)  49-Kuvunja haki za wazazi au kuwaudhi wazazi. 50-Kufanya uchawi na mambo yatenganishayo kati ya mume na mke, au kufanya mambo ambayo yatapelekea mmoja wapo kumpenda mwenziwe bila ya hiari yake.

51- Kula mali ya watu kwa batili. 52-Kutakabari katika Ibada au kujiona ni mwenye kuabadu sana. 53-Kufanya ghushi (Udanganyifu). 54- Kuimba nyimbo na kuzisikiliza. 55-Kubadilisha au kugeuza na kubadilisha usia. 56-Kuwa na ghadhabu ipelekeayo kufanya haramu. 57- Kusengenya na kusikiliza usengenyaji. 58-Kufanya ufisadi katika Ardhi. 59-Kufitinisha. 60-Kueneza ufuska na uovu.

61-Kuuza msahafu mtukufu. 62-Kumuuzia silaha kafiri mwenye kuwapiga vita Waislaam. 63-Kupiga ramli kwa ujumla wake. 64-  Kucheza kamari na kucheza chesi na Drafti hata kama katika uchezaji huo hakutakuwa na kuwekeana rehani. 65-Kukata sala ya wajibu. 66-Kuapa kiapo kiovu na cha uongo. 67-Kufukua Kaburi. 68-Kukata udugu na ujamaa. 69-Kumjaalia Mwenyezi Mungu watoto. 70-Kupiga ramli.

71-Kutoa fatwa bila kuwa na elimu. 72-Kuwapotosha watu kunako njia ya Mwenyezi Mungu. 73-Kuua bila ya haki. 74-Kumuoza au kuoa mwanamke alie haramu kwa sababu ya Nasabu au Kunyonya ziwa moja au  kwa sababu ya ukwe. 75-Mwanamume kumuoa mwanamke ambae ni mahramu wake vilevile. 76-Kupinga na kukataa  kwenda kwenye jihadi. 77-Kukimbia kwenye uwanja wa vita. 78-Kukufuru. 79-Kufanya biashara kwa kitu ambacho ni haram kukifanyia biashara. 80-Kupunguza kipimo na mizani.

81-Kuficha ushahidi. 82-Kuficha ukweli (Haki). 83-Kutaja sifa na uzuri wa Mwanamke mwenye kujihifadhi na kuto fanya maovu pia kijana kwa ujumla. 84-Kutaja aibu za Muumini katika mashairi na mfano wa hayo. 85-Kufunua uchi kwa mwenye kuangalia na mwenye kuheshimiwa. 86-Kulawiti. 87-Upuuzi na michezo ya kipuuzi kwa sura ya ujumla. 88-Kugusa mwili wa mtu mwingine ambae ni ajinabii sawa awe mwanamke au mwanume. 89-Kumgusa mtu mwingine asie kuwa kati ya mke na mume  vijakazi mwenye kumilikiwa na alie halalishwa kwake awe mwanamume au mwanamke mutlaqa kwa matamanio. 90-Kutumia vileo mutlaqa kunywa kunywesha kuuza kununua kulimi na kupandikiza miti ya vileo kwa lengo hilo na kutengeneza vileo na kutumia pesa zitokanazo na vileo na kumpelekea mtu vileo hivyo na kukodisha duka kwa ajili ya kuuza vileo au usafiri wa kusafirisha vileo au kitu kingine kwa ajili ya kusafirisha vileo pia matumizi mengineyo ya vileo kama kuvitumia kutibia majeraha bila ya kuwepo dharura ya kufanya hivyo na mfano wa hayo.

91-Kukhalifu na kwenda kinyume na nadhiri. 92-Kufanya mambo yaliyo haramishwa kwa mwenye kuvaa ihram. 93-Kwenda kwa mpiga ramli na mchawi na kuhani na wenye kutumia mambo ya kimazingara kwa kuvifanya vitu viwe chini ya utumishi wao kama majini na wenye kufanya mazingaombwe na mwenye kuhukumu kwa kuangalia kwenye maji au kioo au Beseni au kwa kuangalia Kucha au Yai na mfano wa hivyo au kwenda kwa watu wenye kumfanya mtu alale kama kumlisha madawa ya kulevya na mwenye kuvuta roho na mfano wa watu hawa watoao khabari  kupitia vitu hivi na mfano wa hivi. 94-Kusuhubiana wanawake wao kwao kwa matamanio. 95-Pia wanamume kusuhubiana wao kwa wao kwa matamanio. 96-Kuzuia kutolewa au kukataa  kutoa Zaka au Khumsi au haki zingine za wajibu. 97-Kuchelewesha kutoa haki au kulipa haki hizo.98-Kupeana mkono kati ya mwanamume na mwanamke ambao ni ajnabii (wasio kuwa ndugu na wanao weza kuoana). 99-Kumjadili Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w) kwa kiburi. 100- Kumjadili Mwenyezi Mungu na Mtume wake na watawala (Ulul amri).

101-Kumtia Mtume (s.a.w) mashakani  na kwenye  matatizo. 102- Kukufuru na hasa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu mtukufu 103- Kuchungulia kwenye nyumba ya jirani. 104-Kukaa kwenye meza yenye pombe. 105-Kukataza mambo mema. 106-Kuingia katika utumishi wa madhalimu. 107-Kuvunja heshima ya nyumba tukufu Al-kaabah au moja kati ya mambo matukufu katika ya dini. 108-Kukata tamaa na kuto kuwa na matumaini na  Rehma za Mwenyezi Mungu. 109-Kurukuu na kumsujudia asie kuwa Mwenyezi Mungu mtukufu. 110-Kuapa kwa kujitenga na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w) au maimamu (a.s) au kujitenga na dini ya Mohammad (s.a.w). 111-Kuchukua utawala kwa njia isiyo ya kisheria. 112-Kumuadhibu mtu ili akiri juu ya jambo fulani.

      Baada ya haya ni jambo lililo wazi kuwa baadhi ya mambo ya haram yaliyo tajwa yanaingiliana yenyewe kwa yenyewe au yanajirudia lakini kutokana na  ukweli kuwa masisitizo yake ni makali au kutokana na kuwa yameelezwa katika aya au riwaya nasi tumeyataja.

    Na ni jambo lililo wazi pia ya kuwa baadhi ya mambo yaliyo tajwa ni Kufru na mengine ni shirki na mengine ni katika madhambi makubwa na mengine ni sababu ya kutoa kafara na kuadhiriwa na kupigwa hududi kama ulivyo elezwa ufafanuzi wake mahala pake katika vitabu vikubwa na vilivyo elezea kwa upana mambo hayo.

 

TABIA MBAYA NA ZENYE KUCHUKIZA

 Kuna mambo na tabia kadhaa ambazo ni mbaya na inampasa Muislaam kuzihama na kujiepusha nazo, nazo ni nyingi sana na maulamaa wa Akhlaq wamezitaja katika vitabu vyao na sisi hapa tutataja zilizo nyingi  japokuwa zingine ni haramu kisheria:

1-Kulipiza kisasi kwa kuvuka mipaka. 2-Kujifakharisha. 3-Kuwaudhi watu wengine hata kama si haramu kama ikiwa mtu atajenga nyumba ndefu zaidi kuliko jirani yake kiasi kwamba hupunguza kufika kwa mwanga wa jua au hewa kwenye nyumba ya jirani yake. 4-Kuwahini na kuwadharau watu, dharau ambayo haijafikia kwenye kiwango cha kuwa haramu. 5-Kuwadharau watu. 6-Kuwatia hofu na kuwaogopesha kwa njia zisizo za haramu. 7-Kufichuia na kueneza mambo ambayo ni vema kuyaficha. 8-Kusema uongo katika mizaha. 9-Kuwacheza shele (kuwafanyia istihzaa) watu. 10-Kuvuka mipaka katika haki za watu wengine kama kukaa mkao wa kukunja nne katika majlisi na kikao ambacho nafasi yake ni finyu.

11-Kutegemezeana katika kufanya mambo ya kheri. 12-Kuzua uongo katika mizaha kama kusema fulani ni mlafi. 13-Kuzungumzia mambo yasiyo mhusu. 14-Kujitegemeza kwa watu. 15-Kufanya matendo ya kipuuzi. 16-Kufanya ujasusi ki siri katika mambo yasiyo muhusu. 17- Kulia kwa kusema maneno yasiyo faa katika msiba. 18-Kusimama kishupavu na kufanya mambo yaliyo kemewa na yenye kuchukiwa. 19- Kuhuzunikia mambo yaliyo pita ya kidunia. 20-Kuto jali mambo ya Akhera.

21-Kupenda kusifia sana kupita kiasi. 22-Kupenda uongozi na cheo. 23-Kupenda mali kupita kiasi. 24-Kupenda Dunia. 25-Kufanya husuda kwa kiwango ambacho hakija fikia kwenye uharamu. 26-Kuwa na pupa. 27-Kuwatupia watu wengine mizigo au matatizo yako binafsi. 28-Kuwa na Hikidi. 29-Kuwaogopa watu. 30-Kujitumbukiza kwenye mambo mabaya.

31-Kujifunga na mambo ya kidunia kama kujifunga na aina ya ulaji au vyakula  (yaani hima yako ikawa ni kuhusiana na mambo ya kula tu) mavazi nyumba na mengineyo kati ya mambo ambayo hayaangaliwi na watu wenye kupenda mambo mazuri na neema. 32-Kukhalifu ahadi (waadi). 33-Kujionyesha hata kama si katika mambo ya kiibada. 34- Kuwa na dhanna mbaya na Mwenyezi Mungu. 35-Kuwadhania vibaya au kuwa na dhanna mbaya na watu. 36-Kuwa na tabia mbaya. 37-Kukaa vibaya na watu. 38-Kujishughulisha na mambo mabaya ambayo si haramu. 39-Kuto ridhia ugawaji wa Mwenyezi Mungu au alicho kupa Mwenyezi Mungu. 40-Kuwa na mahusiano na watu walio duni.

41-Kulialia hali kutokana na mambo ya kimaisha. 42-Ubakhili. 43- Kupitukia katika mambo ya kihayawani. 44-Kuto watakia watu mambo ya kheri hata kama si haramu. 45-Kuidharau nafsi na kuitweza.

46-Kuwadharau watu wengine. 47-Kuwa na nia mbaya au himma mbaya. 48-Kujipiga kama ambavyo baadhi ya watu wamezowea kufanya. 49-Kuwa na tamaa. 50-Kulala sana.

51-Kuwa na matarajio ya muda mrefu. 52-Kuto kuwa na ghira (wivu). 53-Kuwa na ghera au wivu mahala pasipo takiwa. 54- Kuwa na haraka katika mambo. 55-Kufanya uadui kwa kiwango ambacho si haramu. 56- Kuwa na dhanna nzuri na nafsi. 57-Kuwa na asabia na kupenda kwa kijahili. 58-Kuto waheshimu wakubwa. 59-Kuto wahurumia wadogo. 60- Kuto mtegemea Mwenyezi Mungu.

61-Kuchukia bila sababu ya kisheria. 62-Kuwa tajiri sana utajiri ambao huwa ni sababu ya mtu kuwa muovu na kupitukia kwenye maovu. 63-Kuwa na ghuruur (udanganyifu wa kinafsi). 64-Kuwa katika kughafilika na dunia. 65-Kujijutia kwa mambo ya watu. 66-Kuwa na kauli mbaya hata kama haikufikia katika kiwango cha haramu. 67- Kuzusha fitina. 68-Kuwa na moyo mgumu. 69-kubabaika na kuto kiri. 70-Kuwa na kiburi au kutakabari.

71-Kuficha haki hata kama kuidhirisha hakukuwa ni wajibu hata kama kuficha huko ni kwa kunyamaza. 72-Kujiona ni mtendaji sana wa kheri. 73-Kuziona kheri za mwenziwe kuwa ni chache. 74-Kuwaona wenziwe ni watendaji sana wa shari. 75-Kujiona yeye kuwa ni mchache wa kutenda mambo ya shari. 76-Kukufuru neema za Mwenyezi Mungu. 77-Kuto shukuru. 78-Kufanya mizaha sana. 79-Kuto wiana kati ya dhahiri yake na baatini yake (ndani yake) hata katika mambo ya kidunia. 80- Kuto kuwa na haya (kuwa na ushupavu wa kufanya maasi.

81-Kujitenga na waumini. 82-Kuto penda kufanya kazi (kukaa bila kufanya kazi). 83-Kucheka sana. 84-Kuwa na wasiwasi sana hata katika mambo ya kidunia. 85-Kujishughulisha sana na mambo ya kimaisha. 86- Uchafu na kuto chunga usafi. 87-Kutoa kuwa na insaaf (uadilifu). 88- Kuvuka mipaka katika mambo 89-Kuvuka mipika zaidi katika mabo pia. 90-Kukaa pamoja na wafanya maasi.

 91-Kukunja uso bila ya sababu. 92-Kuto jali mambo ya sunna. 93- Kutoacha kufanya mambo ya makruhu. 94-Kuto jali ayasemayo na yasemwayo kuhusiana na yeye. 95-Kuto tilia umuhimu hukumu za kisheria.

 

TABIA (MAADILI) BORA NA MAMBO MAZURI 

Kuna tabia ambazo ni bora na mambo yenye kusifiwa  na ambayo Uislaam umeyahimiza na kuyapendekeza na kuamrisha kujipamba na kusifika na mambo hayo, kiasi kwamba inampasa kila Muislaam kujipamba na mambo hayo nayo ni mengi sana na sisi hapa tutataja kiasi kidogo tutakacho weza katika ya mambo hayo:

1-Kuwa na matumaini na ahadi ya Mwenyezi Mungu mtukufu. 2- Kufanya mambo kwa utuvu na kutofanya haraka katika utendaji wa mambo. 3-Kuidhalilisha nafsi mbele ya Mwenyezi Mungu. 4-Kuwa na insaaf (uadilifu). 5-Kuto wahitajia watu (kujitosheleza). 6-Kujitolea. 7- Kutoa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu. 8-Kuwasaidia watu. 9- Kuizoweza nafsi katika mambo mazuri. 10-Kuamrisha mambo mema.

11-Kukataza na kuzuwia mambo mabaya. 12-Kufanya usuluhishi kati ya watu. 13-Kuwa na Ikhlas (kumtakasia nia Mwenyezi Mung) katika matendo. 14-Kujilewaza na Mwenyezi Mungu. 15-Kuwafanyia wema wazazi wawili. 16-Kuwa na unyenyekevu. 17-Kutembeleana 18-Kuwa na maingiliano na maelewano na watu. 19-Kutubia hata katika mambo ambayo si ya haramu katika ya mambo yamkasirishayo Mwenyezi Mungu mtukufu. 20-Kusalimu amri mbele ya amri za Mwenyezi Mungu katika kila jambo.

21- Kumtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu. 22-Kuwa thabiti na kutoteteleka katika kufanya mambo mema. 23-Kuwa mpole. 24-Kuwa na tabia njema. 25-Kulinda haki za jirani. 26-Kumpenda Mwenyezi Mungu na alie amrishwa na Mwenyezi Mungu kupendwa. 27-Kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. 28-Kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.    

29-Kumuogopa Mwenyezi Mungu. 30-Kuwa na matarajio na Mwenyezi Mungu. 31-Kuogopa madhambi. 32-Kutojitegemeza kwenye matendo. 33-Kuwa na maingiliano na watu. 34-Kuwa na mpangilio mzuri na nafsi. 35-Kuwa na maelewano na mpangilio mwema na watoto na mke. 36-Kuridhia ugawaji wa Mwenyezi Mungu. 37-Kuwa na Zuhdi (kuto ielekea dunia) 38-Kuwa mkarimu. 39-Kuwasitiri aibu za watu. 40- Kurekebisha aibu za nafsi.

41-Kuwa na ulimi mzuri au kauli njema. 42-Kushukuru neema uzipatazo. 43-Kuwarekebisha na kuwasuluhisha watu kwa hekima na mawaidha mazuri. 44-Kuwa na bashasha usoni mwako. 45-Kutoa sadaka kwa wingi na kuwasaidia wanyonge. 46-Kuunga udugu au ujamaa.

47-Kuwatolea watu salam. 48-Kuwatembelea wanyonge wagonjwa na mayatima.  49-Usafi.  50-Kusitiri aibu za watu.

51-Kuwa sawa kati ya dhahiri na batini (ndani) katika mambo yote. 52-Kuwa mkweli na kujiepusha na uongo hata katika mambo ya mizaha na utani. 53-Kuwa na subira (uvumilivu). 54-Kuwakaribisha waumini nyumbani kwako. 55-Kuitika mwaliko wao. 56-Kutuma zawadi katika sehemu zijulikanazo pia kupokea zawadi. 57-Kuwasamehe watu. 58- Kujikinga na mambo ya kijinsia (kuwa na Iffa). 59-Kufanya uadilifu katika kila kitu. 60-Kuwatukuza na kuwaheshimu watu wenye dini.

61-Kujiepusha na mambo machafu na mabaya. 62-Kuwa na ghera (wivu). 63-Kuwapenda mafukara. 64-Kupigana jihadi ya nafsi. 65- Kuwakopesha watu. 66-Kukidhi na kutatua matatizo na haja za waumini. 67-Kuto waudhi waumini au kuzuwia wasifikwe na maudhi. 68-Kuficha siri na kuto itoa nje. 69-Kuwataja watu kwa kheri au kwa wema. 70- Kuharakia kufanya mambo ya kheri.

71-Kuihesabia nafsi juu y ambo iliyo yatenda. 72-Kuwanasihi waumini kwa kutaka kwao ushauri au bila kutaka ushauri. 73-Kuwa na nia ya kufanya kheri au kuwa na nia njema. 74-Kuisafisha nafsi na kuiondolea mambo machafu na mabaya. 75-Kuwa na Taqwaa (kuwa mcha Mungu). 76-Kujikinga na mambo yaliyo haramishwa na Mwenyezi Mungu. 77-Kujiepusha na mambo ya shubha. 78-Kuwa na subira katika kufanya maasi (yaani kuwa na subira na kuto tenda maasi).79-Kuwa na subira juu ya Utiifu wa Mwenyezi Mungu (yaani kubakia kiatika utiifu na kuto muasi Mwenyezi Mungu). 80-Kukumbuka kifo (mauti) na Akhera. 81-Kuwa na Kanaa’a (kuwa ni mwenye kutosheka). 82-Kuwa na haya (Aibu). 83-Kuwa na uso mkunjufu.

KUHUSU TAWBA NA KUREJEA KWA MWENYEZI MUNGU

Imepokelewa kutoka kwa Mtume (s.a.w) ya kuwa amesema: Hakuna siku yoyote ambayo alfajiri yake huchomoza wala usiku wowote ambao giza lake hutoweka isipokuwa huwa kuna malaika wawili wakijibizana kwa sauti nne, mmoja wao akisema: Layti viumbe hawa wasinge umbwa.

Na mwingine husema: Layti pindi walipo umbwa wangelifahamu kwani wameumbwa.

Yule mwingine husema: Na layti wao kutokana na kutofahamu kwao kwa nini wameumbwa wange tenda yale waliyo yafahamu.

Yule mwingine husema: Na layti  wao wakati ule amabapo hawakufanya waliyo yafahamu wange tubia kutokana na yale waliyo yafanya.

Na imepokelewa kutoka kwa Amirul-muuminiin (a.s) wakati mtu mmoja aliposema Astaghfiru llah akiwa mbele yake, Imam (a.s) akasema: Mama yako akulilie unajua istighfaru ni nini? Hakika istighfaru ni daraja ya watu wa daraja ya juu kabisa nayo ni jina ambalo lina maana sita:

Ya kwanza yake ni kujutia makosa yaliyo pita. Na ya pili kuazimia kutorudia makosa hayo kamwe. Na ya tatu Kuwarudishia viumbe haki zao ili ukutane na Mwenyezi Mungu ukiwa ni mororo na mweupe hakuna  deni lolote juu yako. Na maana ya nne ni kukusudia kutekeleza kila jambo lililo faradhi juu yako ambalo ulilipoteza na kuto litekeza na kutekeleza au kulipa haki yake. Na maana ya tano ukusudie kuiyayusha nyama ambayo iliota kwa kula mali ya haramu kwa kuhuzunika mpaka ngozi ishikamane na mifupa na kisha iote nyama nyingine mpya. Na maana ya sita uuonjeshe mwili machungu ya kumtii Mwenyezi Mungu kama ulivyo uonjesha utamu wa maasi, wakati huo unayo haki ya kusema: Astaghfirullah. [11]

Na imepokelewa katika Hadithi nyingine: Mwenye kuazimia kufanya maovu asiyafanye kwani huenda mja akafanya ovu na Mola alie tukuka na mtukufu kumuona na akasema: Nina apa kwa izza yangu na utukufu wangu sinto kusamehe baada ya makosa haya milele. [12]

Na imepokelewa kutoka kwa Imam Swaadiq (a.s) amesema: Ogopeni madhambi yenye kudharauliwa hakika madhambi hayo hayasamehewi, nikasema: Na niyapi hayo madhambi yenye kudharauliwa, akasema: Ni pale mtu anapo tenda dhambi kisha akasema: Ni uzuli ulioje kwangu mimi ikiwa sina dhambi nyingine  tofauti na hii. [13]

Na imepokelewa kutoka kwa Amirul muuminiin (a.s) amesema: Dhambi kubwa ni ile iliyo dharauliwa na mwenye nayo.[14]

Na imepokelewa kutoka kwa Imam Swaadiq (a.s) amesema: Hapana, nina apa kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hakubali twaa yoyote ya mja ikiwa ni mwenye kuendelea kumuasi au ni mwenye kuendela kufanya kiasi kidogo cha maasi. [15]

SALA YA USIKU NA FADHILA ZAKE

Hakika yamepokelewa masisitizo mengi na makubwa juu ya sala ya usiku katika riwaya zilizo pokelewa kutoka kwa maimam (a.s) nayo ni sala yenye rakaa kumi na moja: Rakaa nane ni za sala ya usiku na Rakaa mbili za Shaf’i na Rakaa moja ya Witri na wakati wa sala hiyo ni baada ya nusu ya usiku hadi kuchomoza kwa alfajiri. Na kila baada ya rakaa mbili hutoa salam isipokuwa rakaa ya Witri hakika rakaa hiyo pekee inasalam na ni sunna kusoma Qul-huwallahu Ahad mara thalathini katika kila rakaa moja kati ya rakaa mbili za mwanzo na katika rakaa zilizo bakia ni sunna kusoma sura ndefu kama suratul-An-aam na suratul- Kahfu na suratul- Anbiyaa na sunna hii itafanyika ikiwa wakati wake ni mpana.

Na ni sunna kusoma sura ndefu katika rakaa ya mwanzo na sura fupi katika rakaa ya pili na vilevile ni sunna kusoma suratul- Falaq na An-nnas na Tawhiid katika rakaa za Shaf’i na Witri au Qul-huwallahu Ahad katika rakaa zote. Na katika kunuut ya rakaa ya Witri  anawaombea waumini arobaini na unasema:

Ewe Mwenyezi Mungu msamehe fulani na kutaja jina la yule muumini badala ya neno (Fulani) na mtoto usimuhesabie katika hao watu arobaini na ni sunna pia katika kunuut kusoma istighfar mara sabini na bora zaidi ni mara mia moja na kuinua mkono wake wa kushoto katika kunuut wakati akisoma istighfar na kuhesabu kwa mkono wake wa kulia na kilicho bora zaidi katika namna ya kusoma istighfar aseme: Ninamuomba Mwenyezi Mungu msamaha Kutokana na dhulma yangu yote niliyo ifanya na makosa yangu yote na uharibifu nilio ufanya katika mambo yangu na ninatubia kwake.

( أستغفر الله من جميع ظلمي و جرمي وإسرافي في أمري و أتوب إليه)         

Na inatosha akisema: Ninamuomba Mwenyezi Mungu msamaha ambae ni mola wangu na ninatubia kwake.

( أستغفر الله ربي و أتوب إليه)

Na ni sunna kusema mara saba: ( هذا مقام العا ئذ بك من النار)  na vilevile ni sunna kusema mara mia tatu: (العفو ) na akitaka kuunganisha herufi ya waw ni lazima aiwekee fatha.

Na inatosha kuzifahamu fadhila zake kwa kuisoma riwaya iliyo pokelewa: Ya kuwa Mwenyezi Mungu alimtelemshia Mussa wahyi na kusema: Simama katika usiku wa kiza, na lifanye kaburi lako kuwa ni bustani kati ya mabustani ya peponi. [16]

Na imepokelewa kutoka kwa Amirul muuminiin (a.s) amesema: Kusimama usiku ni Afya kwa mwili. [17]

Na imepokelewa kutoka kwa Imam Swaadiq (a.s) amesema: Sala ya usiku huupendezesha uso au huufanya uso kuwa mzuri na huifanya tabia iwe njema na huifanya harufu kuwa nzuri na kuongeza riziki na hulipa deni na huondoa himma na kuondo pazia katika macho. [18]

Na imepokelewa kutoka kwake pia (a.s): Ameongopa mwnye kudai ya kuwa anasali sala ya usiku hali ya kuwa ni mwenye njaa, hakika sala ya usiku inampa mtu dhamana ya rizki yake ya mchana. [19]

 

BAADHI YA ADABU ZIFANYWAZO MTOTO ANAPO ZALIWA

Kuna mambo ambayo ni sunna kufanywa  mtoto anapo zaliwa na tutashiri na kuyagusia mambo hayo kupitia mambo mawili yafuatayo:

JAMBO LA KWANZA

Ni sunna kumuosha mtoto baada ya kuzaliwa na kumuadhinia kwenye sikio lake la kulia na kukimu kwenye sikio lake la kushoto na kumpaka mtoto maji ya mto Furati na kumuita jina katika siku ya saba, na ni sunna kumnyoa kichwa chake katika siku hii na kutoa sadaka ya Dhahabu au Fedha  kulingana na uzito wa nywelie zake, na kama hakunyolewa katika siku hii sunna hii ina anguka, na ni sunna kumchinjia mbuzi au ngamia katika siku ya saba na kila mnyama anavyo kuwa mkubwa na mzuri ndivyo inakuwa vizuri zaidi, na ni sunna mkunga kutengewa mguu na paja na kama hakuwa na mkunga basi nyama hiyo hupewa mama mzazi hisa ya mkunga nae kumpatia amtakae, na kama mkunga atakuwa ni yahudi asie kula nyama iliyo chinjwa na Waislaam atapewa robo ya  thamani ya mbuzi, na ni sunna kutoa sadaka baadhi ya nyama ya mnyama huyo na iliyo bakia kuipika na kuwakaribisha waumini kumi  na zaidi ya kumi ni bora zaidi.

Na ni sunna kumtaili (kumkhitani) mtoto katika siku ya saba na kama hakumtaili walii wake ni wajibu kwake mwenyewe mtoto akifikia balee kujitaili.

Na ni sunna kusoma Dua hii ifuatayo wkati wa kumtaili:

اللهم هذه سنتك وسنة نبيك (ص) و اتباع منا لك و لنبيك بمشييتك و بإ راد تك و قضائك لامر انت اعرف به مني, اللهم فطهره من الذنوب و زد في عمره وادفع الآافات عن بد نه و الاوجاع عن جسمه و زده من الغني و اد فع عنه الفقر, فإنك تعلم و لا نعلم        

Na imepokelewa kutoka kwa Imam Swaadiq (a.s) ya kuwa ni sunna kumsomea mtoto dua hii kabla ya kufikia balee ikiwa haikusomwa wakati wa kumtaili hakika Mwenyezi Mungu humuondole mtoto huyo makali na machungu ya chuma katika kuuwawa na mengineyo.

Kisha ikiwa hakuchinjiwa siku ya saba ni sunna kumchinjia hadi mwisho wa umri wake bali hata kama atafariki, na mwanamume achinjiwe mbuzi dume na mwanamke achinjiwe jike na chini ya hapo ni dume mutlaqa (vyovyote itakavyo kuwa sawa awe mwanamume au mwnamke) na ikikosekana basi chochote kitakacho thibitisha kuwa amefanyiwa Akika na haishurutishwi katika Akika masharti ya mnyama wa kuchinjwa kwenye hijja (Al-udh-hiya) na lau kama hakupata Akika atasubiri na haitoshi kutoa sadaka thamani ya mnyama wa Akika.

Kwa msingi huu ni jambo lililo wazi kwamba inajuzu kwa baba na mama na wengineo kula nyama ya Akika ya mtoto wao lakini ni makruhu kwa baba na mama kula nyama hiyo, bali ni makruhu kila ambae yuko chini ya uangalizi wa baba,  na mama kula nyama hiyo umakruhu wake ni mkubwa zaidi.

Kisha kilicho bora ni Akika kukatwa vipande vipande na kuto vunjwa mifupa yake, ama kuzika mifupa ya Akika hatukupata dalili inayo zungumzia suala hilo na inajuzu Akika kukatwa na kupewa jirani kama zawadi na wengineo na kilicho bora ni kupikwa na kukaribishwa kundi fulani la waumini.

Na Akika haiwahusu mafukara peke yao bali inajuzu kuwa hata matajiri wenye kujitosheleza vile vile masayyid hata kama alie chinja Akika si sayyid na lau kama baba hakumchinjia mwanae ni sunna kwa mtoto mwenyewe kujichinjia, na kichinjo cha Hajji kinatosheleza kunako Akika na lau kama mtoto atabakia hadi siku ya saba ni sunna kumfanyia Akika na hata kama atafariki baada ya adhuhuri, ama lau kama hakubakia hai hadi wakati wa adhuhuri  wakati huo Akika ina anguka hailazimu kumfanyia akika.

 

JAMBO LA PILI

Hakika chakula bora kabisa kwa mtoto mchanga ni: Maziwa na  maziwa bora kabisa na mazuri kwa mtoto ni maziwa ya mama, lakini si wajibu kwa mama kumnyonyesha bila ya malipo, na malipo ya kumnyonyesha kwake ni juu ya baba yake, kwa hivyo basi inajuzu kwa mama kuchukua malipo kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto huyo japo kuwa lililo bora kwa mama ni kuto chukua malipo, ndio, ikiwa baba atakosa mtu wa kumnyonyesha au haikuwezekana kunyonya sehemu nyingine ni wajibu kwa mama kumnyonyesha mtoto huyo.

Kisha ni kuwa ikiwa mtoto atakuwa na mali inajuzu kwa baba kutoa malipo ya kumnyonyesha kwenye mali yake na si wajibu kwa baba wakati huo kutoa malipo yeye mwenyewe, na ni sunna kwa mama kumnyonyesha mtoto kwenye chuchu zote mbili kwa pamoja na muda kamili wa kumnyonyesha kwa kauli ya ahwat ni miaka miwili na inajuzu chini ya miaka miwili hadi kufikia miezi mitatu na haijuzu kupungua zaidi ya hapo isipokuwa kwa dharura, na kauli ya ahwat ni kuto zidisha miaka miwili.

Kwa nsingi huu ni jambo lililo wazi kuwa  mama  kumnyonyesha mtoto wake katika muda ulio tajwa ikiwa atamnyonyesha bila ya malipo yoyote, au akachukua malipo kwa kiwango kichukuliwacho na wengineo wenye kunyonyesha, wakati huo haijuzu kwa baba kumchukua mtoto kutoka kwa mama, ndio ikiwa atataka malipo makubwa zaidi kuliko wengine wakati huo inajuzu kumpatia mtu mwingine wa kumnyonyesha.

Kisha ni kuwa mama anayo haki ya malezi ya mtoto hadi kufikia miaka miwili na ikiwa ni binti ni hadi miaka saba ikiwa mama ni Muislaam huru na mwenye akili timamu na muaminifu na hakuwa na mume mwingine, wakati huo haijuzu kwa baba kumchukua mtoto kutoka kwa mama katika muda huo ulio tajwa, ama baada ya muda ulio tajwa hakika haki ya malezi inakuwa ni ya baba, na ikiwa baba atafariki haki hiyo inarejea kwa mama kwa kauli ya ahwat na wasii hatamzaahim wala kumtia bughudha  mama na Mwenyezi Mungu ndie mwenye kujua.

Na hapa ndio mwisho wa yale tuliyo kusudia kuyatoa kwa muhtasari hapa kati ya pande kuu za mafunzo ya juu ya  kiisalaam, ninakusudia: Elimu ya Usulud-dini na Furuud-dini na elimu ya Akhlaq (Tabia au Maadili) na adabu za kiislaam na ambayo ni wajibu (waajibul aini) juu ya kila Muislaam wa kike na kiume kujifunza mafunzo hayo na kuyafanyia kazi, ili tuweze kupata hadhi nzuri na tuweze kufanikiwa katika dunia yetu kwa kuishi maisha mema na yenye raha tele na kufaulu katika Akhera yetu kwa kupata pepo ya daima na yenye kubakia milele  inshaa allah taala na Mwenyezi Mungu ndie mwenye kutoa tawfiiq na msaidizi juu ya yote hayo.


[1] - Mustadrakul-wasaail: Mujallad wa 11/ 187.

[2] Suratul qalam aya 4.

[3] Suratu Aal-imraan ya 159.

[4] Suratush-shuraa aya 89.

[5] Suratul-baqara aya 83.

[6]- Buharul-anwaar: Mujallad wa 32/561.

[7]- Suratul-Aaraaf aya 199.

[8]- Suratul-furqaan aya 63.

[9] Suratun-nahli aya 90.

[10] Suratul-an’aam aya 151.

[11] - Buharul-anwaar: Mujallad wa 6/36, mlango wa 20, hadithi ya 59, ikinukuliwa kwenye kitabu Nahjul balagha.

[12] Rawdhatul-waaidhiin: Ukurasa 479, Majlisi fii Dhikrit-tawbah.

[13] Wasaailush-shia: Mujallad wa 11/ 245, mlango wa 43, hadithi ya 1 .

[14] Nahjul balagha Qiswarul-hikam: ukurasa 21 na Qiswarul-hikam: Ukurasa 477.

[15] Wasailush-shia: Mujallad wa 11/ 268, mlango wa 48 hadithi wa 1.

[16] Mustadrakul-wasailush-shia: Mujallad wa 6/331.

[17] At-tahdhiib: Mujallad wa 2/121.

[18] Wasaailush-shia: Mujallad wa 8/152.

[19] Wasailush-shia: Mujallada wa 8/158.