SEHEMU YA PILI

 MATAWI YA DINI

Kabla ya kuanza kubainisha na kufafanua sehemu ya pili katika mafunzo ya juu ya Uislaam, hapana budi

kuashiria hapa ya kuwa sehemu ya kwanza ya mafunzo ya kiislaam ya hali ya juu na yaliyo matukufu yaani: Usulud-dini ambazo tumezi zungumzia, ni lazima mwanadamu aziitakidi au awe na itikadi nazo-kwani misingi hiyo ndio inayo husiana na ukafiri na itikadi- kutokana na ijtihadi na kwa kutegemea dalili na wala haitoshi kwenye misingi hiyo kujitegemeza sehemu fulani au kwa mtu fulani na kumfuata mtu huyo.

Wakati ambapo Furuud-dini (matawi ya dini), ambayo hivi sasa tuko mbioni kuyafafanua na kuyazungumzia, hakika matawi hayo yameenea na kuzihusu sehemu na nyanja zote za maisha  na yanazihusu harakati zote za mwanadamu  na matendo yake yote kabla ya kuzaliwa kwake mpaka baada ya kufariki kwake na maranyingi mwanadam-kwa sababu ni mambo yanayo husiana na matendo kama harakati za mwanadamu na kutulia kwake na utendaji au utekelezaji wa mambo ya aina tofauti na mabadiliko-hawezi kufanya ijtihadi (kujitahihi) katika mambo yote hayo na kufahamu hukumu zake kutokana na dalili zake kwa uchambuzi wake ulio tajwa katika vyanzo vine vya sheria: Qur'ani tukufu, Sunna sharifu- Yaani hadithi za Mtume (s.a.w) na riwaya za Ahlul bayti (a.s)- na Ijmaa (Makubaliano ya wanazuoni) na Akili, kwa hivyo Uislaam ukajuzisha (ukamruhusu) kwa mwanadamu kumfuata mujtahidi alie kusanya masharti ya kufuatwa (kufanyiwa taqliid) kwenye mas'ala hayo na kurejea kwake katika mas'ala hayo kwa ajili ya kumfanyia wepesi na kumrahisishia mambo.

Ndio, hakika matawi ya dini ni mengi sana na sisi tuta ashiria yale yaliyo muhimu sana nayo ni kumu yaliyo maarufu, kisha tutabainisha na kufafanua yale ambayo yanahitaji kufafanuliwa kati ya hayo inshaa allah taala ama matawi hayo kumi yaliyo maarufu ni kama yafuatayo:

1-Sala

2-Saumu (Funga)

3-Khumsi

4-Zaka

5-Hajji

6-Jihadi

7-Kuamrisha mema

8-Kukataza maovu

9-Kuwatawalisha mawalii wa Mwenyezi Mungu

10-kujhitenga na kujiepusha na maadui wa Mwenyezi Mungu

Kwa kuyafahamu hayo ni jambo lililo wazi kuwa matawi haya pamoja na kuongezea matawi mengine kama uuzaji (bayii) na ununuzi na Nikah (Ndoa) na Talaka, Kisasi na Diyaa (fidia), hayo yamefafanuliwa na kufanyiwa bahthi kwa upana zaidi katika kitabu hiki-katika kifungu cha masaail-lakini baadhi yaliyo muhimu kati ya hayo yamebakia na ambayo ni katika mambo yaliyo sambamba na yenye kuwiana na zama hizi tunazo ishi, kama jamii ya wanadamu na nidhamu ya kijamii na kisiasa, Uchumi,  Jeshi na nguvu zadola, kama Jeshi la ulinzi na polisi, Mahakama na utoaji hukumu, Utamaduni na Vyombo vya habari, Afya na nyenzo za tiba, Uhuru wa kila mtu mmoja mmoja na uhuru wa jamii na mengineyo, haya ndio ambayo tutayazungumzia katika sehemu hii kwa utashi wake Allah.

 

JAMII NA  DOLA (NIDHAM) LA KIISLAAM

 Hakuna shaka ya kuwa Uislaam unayo nidhamu maalum ya utawala na uendeshaji wa mambo ya kijamii, kama ambavyo hakuna shaka ya kuwa nidhamu hii maalum  ya kiislaam imekuwa ikitekelezwa katika nchi za kiislaam kwa muda wote wa karne kumi na tatu (13) mpaka lilipo anguka dola la kiislaam kabla ya zaidi ya nusu karne –sawa utekelezaji huo ulikuwa  ni utekelezaji kamili wa kanuni zote au ulikuwa ni utekelezaji pungufu-

Kisha mtu ana weza kusikia ya kuwa utamaduni wa kiislaam (Al-hadharatul- islaamiyyah) ulikuwa ni utamaduni wa aina yake na bora kwa kiwango kikubwa na ulio pituka tamaduni zingine zote, na anaweza kusikia ya kuwa Uislaam-kutokana na hekima za kanuni zake zitokazo mbinguni na zilizo na uadilifu-umebeba jukumu la kutatua matatizo yote ya ulimwengu na kwamba kanuni hizo lau kama zitatumika na kurudishwa kwenye utawala, dunia itabadilika na kuwa pepo yenye neema  na watu kuishi kwenye kivuli na neema zake raha mustarehe, na wangeishi maisha mema na yenye  raha tele.

Kwa msingi huo: Basi nidhamu hiyo ni ipi?

Na je kuna uwezekano wa Nidhamu na Utawala wa kiisalam kurudi tena kwenye uhai katika zama hizi za upanukaji wa dunia na maendeleo ya kianga na maendelo ya atomi na katika zama za maendeleo ya Internet na kupanuka kwa habari na vyanzo vyake?

Na ikiwa Uislaam utachukua Utawala vipi utaweza kutatua matatizo yaliyopo ya kiulimwengu?

Hakika haya ni maswali yanayo paswa kupatiwa majibu……

Na Pengine-majibu ya maswali tutakayo yataja hapa -yaka amsha hali ya mshangao  na kustaajabu  na msomaji kupigwa na butwaa na kudhania ya kuwa sisi tunazungumzia kuhusu mji ulio bora kabisa, pamoja na kuwa sisi tuna maandalizi kamili na tuko tayari kuondoa mshangao huo na kustaajabu huko kwa kutoa dalili na ushahidi wa kiisalaam juu ya majibu hayo,[1] na kutoa mifano hai na ya wazi kabisa kutoka kwenye historia ya utawala wa kiislaam ulio safi na halisi, jambo linalo thibitisha uwezo wa Utawala na Nidhamu ya kiislaam kurudi tena na kwa mara nyingine kwenye uhai na kushika hatamu ya uongozi  na kuendesha mambo kwa ujasiri kamili na kwa umadhubuti bila kuteteleka, kwani Nidhamu ya kiisallam ndio Nidhamu pekee kati ya Nidhamu zote za ulimwengu- kuanzia hizo za zamani na za hivi sasa na zitakazo jitokeza kwa siku za baadae-kutokana na hekima za kanuni na sheria zake zitokazo mbinguni- yenye uwezo wa kuuendesha ulimwengu wenye maendeleo na ulio funguka au ulio wazi, uendeshaji uwezao kuufikisha kwenye matarajio yake na kuyathibitisha  matumaini yake  na kuutatulia matatizo yake na kuuondolea matatizo unayo kabiliana nayo na kuuondolea mambo yanayo usibu kama Uovu Madhara Ujinga Maradhi na kuufikisha ulimwengu huo kwenye ukingo wa Amani na Matumaini na kuufikisha kwenye ufukwe wa sa’aada na Amani, na Nidham hii imekusanya sababu na nyenzo zote za kuuletea maendeleo na kuufisha kileleni na kuyathibitisha yote ayatakayo mwanadamu katika nyanja hizi: kama Siasa Uchumi Uhuru na mengineyo ambayo tutayaelezea kwa muhtasari:[2]

 

 

UISLAAM NA SIASA

SWALI: Je katika Dini ya kiislaam kuna siasa?

JAWABU: Ndio, ndani ya Uislaam kuna sehemu au fungu bora kabisa kati ya mafungu ya siasa na kuna aina nzuri kabisa kati ya aina za idara na uendeshaji wa nchi na wananchi (waja wa Mwenyezi Mungu).

SWALI: Je utawala katika Uislaam ni utawala wa kijamhuri au ni utawala wa kifalme?

JAWABU: Utawala katika Uislaam si utawala wa kijamhuri wala wa kifalme-kwa maana ya kiistilahi ya maneno hayo yalivyo elezwa kwenye kamusi za ulimwengu wa kimagharibi (yaani kama yanavyo elezwa kwenye makamusi ya nchi za magharibi katika zama hizi-bali ni utawala wa mashauriano ya watu na inasihi kuuita kuwa ni utawala wa kijamhuri, kutokana na kuwa ni utawala unao tegemea mashauriano ya wananchi, kwani katika Uislaam hakuna utawala wa kifalme wa kurithishana.

SWALI: Ni zipi sifa za mtawala (kiongozi) wa kiislaam?

JAWABU: Kiongozi wa kiislaam ni mtu muumini, mwenye elimu ya sheria ya dini ya kiislaam kikamilifu na mwenye kufahamu mambo ya kidunia na mwenye kusifika na sifa ya uadilifu kikamilifu, kwa hivyo basi mtu yeyote atakae kamilisha masharti haya na watu wengi kumridhia, basi anakuwa mtawala na akipungukiwa na moja wapo kati ya masharti haya atauzuliwa na kutolewa kwenye cheo chake kwa haraka sana lakini ikiwa umma (watu) hawakuridhia abakie kwenye cheo chake hicho na kuwa raisi, na wanayo haki ya kumbadilisha na kumuweka mwingine alie kusanya masharti hayo.

SWALI: Ni nani anae mteua mtawala wa kiislaam?

JAWABU: Sehemu kubwa ya umma (watu walio wengi) na hii inahusika tu ikiwa mtawala huyo au kiongozi huyo si maasuum alie teuliwa na Mwenyezi Mungu alie takasika na mtukufu kama Mtume na maimamu watwaharifu (a.s)….. 

 

AINA YA UTAWALA NA NAMNA YA KUTAWALA

SWALI: Je katika utawala wa kiisalam kuna suala la uchaguzi na utoaji wa maoni na upigaji wa kura na je kuna bunge la wawakilishi wa watu na vikao vya manispaa na mikoa na mfano wa hayo?

JAWABU: Ndio yote hayo yamo ndani ya Uislaam- hasa katika zama zetu hizi ambazo Imam Mahdiy (a.s) yuko mafichoni (katika Ghaiba)- lakini kwa mfumo wa kiisalaam, kwa mfano: Bunge jukumu lake ni kutekeleza na kufuatisha au kutekeleza kanuni za ujumla kwenye sehemu zake na maswaadiki zake,  na jukumu lake si kuweka sheria mpya na kutunga sheria mpya, kwa sababu utungaji wa sheria na kanuni kwanza kabisa hiyo ni haki ya Mwenyezi Mungu mtukufu na pili ni kuwa hakuna upungufu katika hukumu za kiislaam na wala hakuna kasoro wala upungufu, mpaka tuhitaji kutunga sheria mpya na kutunga kanuni zingine, kwa mfano imepokelewa katika hadithi kwamba: (Hakika Uislaam umetubainishia hukumu za kila kitu hata hukumu ya dia (fidia) ya mkwaruzo) (yaani mtu akimkwaruza mwenziwe kuna hukumu yake) na imepokelewa katika hadithi nyingine ya kuwa: (Halali ya Mohammad (s.a.w) ni halali hadi siku ya kiama na haramu yake ni haramu hadi siku ya kiama)[3]

Kwa hivyo basi: Mtu yeyote hana haki ya kuharamisha jambo fulani na kuhalalisha jambo lingine bali haki yake ni katika kutekeleza na kutenda, kwa mfano: Uislaam umehukumu ya kuwa biashara katika nchi ni haki ya watu na wafanya biashara, kwa hivyo bunge halina haki ya kubadilisha sheria hii au kuibadilisha kwa kuifungamanisha au kuihusisha  na watu fulani tu au kuihusisha tu na serikali, wakati ambapo Uislaam haukuhukumu ya kuwa utembeaji bara barani na majiani uwe kwa upande wa kulia au upande wa kushoto, kwa hiyo katika sehemu kama hizi ni haki ya bunge kuainisha kuwa iwe ni upande wa kulia au kushoto, na imekuwa hivyo kwa sababu Uislaam umeamrisha kuwepo  nidhamu na kuto kuwa na fujo na kila mtu kufanya atakavyo, na suala la kuainisha upitaji wa mabarabarani au njiani iwe ni upande wa kulia kwa mfano ni kutekeleza nidhamu ambayo imehukumiwa na Uislaam  na kuweka sheria yake na hali ni hiyo hiyo katika mambo mengine mfano wa hilo.

SWALI: Sasa kwa nini hivi leo tunaona katika nchi za kiisalam upungufu na matatizo na utungaji wa sheria na kanuni?

AJAWABU: Hakika nchi hizo ni nchi za kiisalaam kwa jina tu na  kwa alama na si zaidi ya hivyo na Mwenyezi Mungu mtukufu amekwisha sema: [4]

(ومن أعرض عن ذ كري فان له معيشة ضنكا ونحشره يوم القيامة أعمي)

(Na mwenye kujiepusha na utajo wangu (Qur'ani) hakika mtu huyo ana maisha ya taabu na siku ya kiama tutamfufua akiwa kipofu)         

Kwa hivyo yule ambae anachukua jukumu la kutunga sheria na kuacha au kujiepusha na hukumu za Mwenyezi Mungu anayafanya maisha yake kuwa finyu na ya dhiki-kama maisha ya nchi za kiislaam yalivyo kuwa finyu-na mtu huyo katika Akhera  ana aibu na moto.

 

 

MAJUKUMU YA UTAWALA WA KIISALAAM

SWALI: Ni lipi jukumu la utawala wa kiisalaam kuuelekea Umma?

JAWABU: Jukumu lake ni kuhifadhi na kulinda uadilifu kati ya watu- ndani ya nchi na nje ya nchi-na kuyafanya maisha yaendelee na kuondoa mahitaji kwa kukithirisha mahitaji ya watu: kuwapatia riziki, mali, kuwapatia elimu na kuwapatia elimu za juu na kuhifadhi Amani na usalama wao na utulivu wao.

SWALI: Ni kanuni ipi ambayo hutekelezwa na dola la kiislaam?

JAWABU: Ni kanuni itokanayo na kitabu na Sunna za Mtume (s.a.w) na Ijamaa na Akili.

SWALI: Ni nani mwenye kuweka kanuni ili ziweze kutekelezeka?

JAWABU: Huwekwa na mafaqihi (maulamaa wa fiqhihi) walio waadilifu ambao ndio marejeo ya Umma yaani wanazuoni wa mambo ya dini na Dunia, ambao watu hurejea kwao katika taqliid.

SWALI: Je katika Uislaam kuna makundi mbali mbali ya kisiasa?

JAWABU: Hakuna shaka kuwepo kikundi ambacho kiko chini ya uangalizi wa maulamaa ambao ndio marejeo ya watu, ikiwa kikundi au chama hicho ni utangulizi wa kuunda bunge la wananchi amabalo ndio linalo takiwa kutekeleza na kufuatilia utekelezaji wa sheria, ama kikundi ambacho kitakuwa ni utangulizi wa kusimamia utungaji wa sheria  hakifai kuwepo na hilo linatokana na ukweli kuwa utungaji na uwekaji wa sheria hilo ni jukumu maalu tu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu alie takasika.[5]

 

UCHUMI WA KIISLAAM

SWALI: Je katika Uislam kuna mfumo maalum wa kiuchumi?

JAWABU: Ndio na ulio bora zaidi kuliko mifumo iliyo wahi kujulikana katika ulimwengu huu.

SWALI: Je mfumo wa kiuchumi wa kiislaam ni wa kibepari (Capitalism) , au kijamaa? au ni wa Makomonisti au ugawaji kwa sawa?

JAWABU: Hakuna Ubepari wala ujamaa katika Uislaam,- kwa maana ifahamikayo hivi leo- na wala si wa kikomonisti wala ugawaji.

SWALI: Basi mfumo wa kiislaam uko je?

JAWABU: Uchumi wa kiislaam unaheshimu umiliki wa mtu mmoja mmoja na unaukiri kwa sharti kwamba umiliki huo usitokane na mali ya haramu, na nisharti kutekeleza na kutoa  haki zake za kisheria.[6]

SWALI: Basio dola (serikali) linapata vipi mapato yake?

JAWABU: Dola linapata mapato yake kwa kukusanya haki za kisheria zilizo thibitishwa ndani ya Uislaam.

SWALI: Ni zipi hizo haki za kisheria zilizo wajibu?

JAWABU: Haki hizo ni nne: Khumsi, Zaka, Kodi za Ardhi, na  Jizya (mali ichukuliwayo kutoka kwa Mayahudi na Wakiristo walio wekaeana mikataba na dola la kiisalaam kwa ajili ya kuwalinda)

 

VYANZO VYA MAPATO KATIKA UISLAAM 

SWALI: Tufafanulieni haki hizi ambazo ndio vyanzo vya mapato katika Uislaam kama mlivyo taja hapo kabla?

JAWABU: "Khumsi" ni mali au pesa ichukuliwayo na mtawala wa kiislaam (Haakim) nayo ni asilimia (20%)  katika faida zote  za kisheria na katika Madini, Mali iliyo fichwa chini ya ardhi, na Mali itolewayo baharini kwa kuzamia, na Mali ya halali iliyo changanyika na haramu na Mali iliyo patikana kwenye vita kati ya Waislaam na Makafiri na sehemu fulani ya Ardhi.

Na "Zaka" ni mali ichukuliwayo na mtawala wa kiisalaam moja ya (40) na moja ya (100), na Zaka huchukuliwa katika Mbuzi, Ng'ombe, Ngamia, Dhahabu, Fedha, Tende, Zabibu, Shairi na Ngano.

Na "Kharaaj" Ni kodi zichukuliwazo na mtawala wa kiislaam kutoka kwa wakulima, katika ardhi zilizo kombolewa bila mapigano au bila kutumia nguvu.

Na "Jizya" ni mali ichukuliwayo na mtawala wa kiisalaam kutoka kwa Mayahudi, Wakiristo na Majusi walio wekeana mikataba, na makafiri wengine kwa ajili ya kuwahami na kuwalinda au kwa ajili ya dhimma fulani.

SWALI: Je katika Uislaam kuna Mabenki?

JAWABU: Ndio lakini mabenki ya kiislaam hayana riba wala nyongeza, kwani riba katika Uislaam ni sawa na kumtangazia vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake, pamoja na kutekeleza sheria zake zote za kiislaam za mali na mambo ya wafanyakazi huendeshwa na mapato mengine na ikiwa hayakutosheleza, basi hukamilishwa kutoka katika hazina (baytul mali) ya dola la kiislaam.

SWALI: Je dola au serikali huchukua mali zingine kutoka kwa watu tofauti na hizo zilizo tajwa, kati ya mafungu yaliyopo hivi sasa?

JAWABU: Hapana, kwani dola la kiislaam halina haki ya kuchukua zaidi ya mafungu manne yaliyo tajwa-kamwe-na imepokewa katika hadithi kama ifuatavyo: (Mwenye kuchukua  mali kwa yeyote bila ya ridhaa yake, Mwenyezi Mungu ataichukua mali hiyo siku ya kiama kutoka kwake, badala ya kila Dirham atachukua sala mia saba kati ya sala zake zilizo kubaliwa na kumpatia mwenye mali).

 

BAYTUL- MAALI YA WAISLAAM

(HAZINA YA WAISLAM)

SWALI: Dola la kiislaam, huzifanyia nini pesa au mali lizichukuazo na kuzikusanya kutoka kwa watu?

JAWABU: Kwa hakika katika dola la kiislaam kuna idara au Wizara kwa istilaha ya kisasa ijulikanyo kwa jina la (Baytul mali) katika wizara hii hukusanya mali yote ikusanywayo kutoka kwa watu na mali hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kutatua mahitaji yote ya Waislaam, pamoja na kuwa dola husimamia mipango yote ya kimaendeleo ujenzi na maendeleo mengine ya nchi, pia hutenga fungu fulani la mali na kumpatia kila fakiri kiasi cha pesa kimtoshelezacho kuendesha mambo yake ya kimaisha, ili asibakie fakiri katika nchi (kwa maana kuwa huweka mpango wa kupiga vita ufukara nchini) na hukidhi haja ya kila muhitaji, kwa mfano mwenye kutaka kuoa, au mtaji wa kuanzisha biashara, au kujenga nyumba na kuanzisha duka, au kwa ajili ya matibabu, au kwa mwenye safari ya lazima kutokana ya haja au tatizo,  au humpatia mtu alie katikiwa na matumizi akiwa safarini na hakuwa na pesa ya kumrudisha nyumbani kwake, au kuwasaidia wanafunzi wanao hitajia pesa katika masomo yao kama kulipia karo, na mfano wa hayo kwa kurejea kwenye baytul mali- na kuithibitishia-kwa njia za kawaida, kama kuleta mashahidi, au kuapa- ya kuwa anahaja ya kitu fulani na hana pesa, wakati huo baytul mali humpatia kiwango kinacho tosheleza kukidhi haja yake kulingana na hadhi yake na chenye kumtosheleza, na kwa msingi huu hakutabakia katika dola la kiislaam fakiri au muhitaji-kamwe-. 

SWALI: Je haki na pesa hizo za aina nne zilizo tajwa zinatosheleza mahitaji yote hayo?

JAWABU: Ndio, inatosha ukiongezea mapato liyapatayo dola la kiisalaam kutokana na ghanima (Ngawira) na imepokelewa katika hadithi ya kuwa: (Lau kama pesa hiyo haikutosheleza basi Mwenyezi Mungu angeongezea katika kiwango chake) (yaani angeongeza katika kiwango kinacho takiwa kutolewa).[7]

 

UCHACHE WA WIZARA NA WAFANYA KAZI

SWALI: Vyanzo vya mapato vilivyo tajwa na ambavyo ni vichache, vinatosheleza vipi wakati tunaona ya kuwa hivi leo kuna vyanzo vikubwa na vingi vya mapato na bado havitoshelezi  mahitaji ya serikali na watu?

JAWABU: Vinatosheleza kutokana na uchache wa muundo wa dola na uchache idara (Wizara) na wafanya kazi wake kuwa waaminifu na mambo kuwaachia watu wenyewe, kwa mfano: Wafanya kazi katika dola la kiislaam ni wachache sana, kwa sababu idara au wizara nyingi dola la kiislaam halina haja nazo, kisha ni kuwa kazi nyingi ambazo husimamiwa na dola na serikali-kwa hivi sasa-husimamiwa na watu binafsi katika dola la kiisalaam na hakubakii katika majukumu ya dola na serikali ya kiislaam isipokuwa kazi chache  kiasi kwamba dola linakuwa na uwezo wa kuzitekeleza kwa haraka sana na kwa urahisi zaidi kadri iwezekanavyo na ni jambo lililo wazi kuwa: pindi idadi ya wafanya kazi inapokuwa chake na mishahara kupanda na mambo ya watu kuwaachia watu wenyewe na wasimamizi  kuwa waaminifu hapo mali hukithiri na kuwa nyingi.[8]

SWALI: Je walio staafu kazi hupewa pensheni?

JAWABU: Ikiwa ni fakiri asie jiweza hupewa kulingana na mahitaji yake, si kwa kiwango maalum-kama ijulikanayo katika serikali na madola mbali mbli ya siku hizi.[9]

 

DHAMANA YA KIJAMII KATIKA UISLAAM [10]

SWALI:Je katika Uislaam kuna dhamana ya kijamii?

JAWABU: Ndio na ni bora kabisa kati ya aina ya  dhamana za kijamii na za kiwango cha juu kabisa.

SWALI: Je mnaweza kutubainishia na kutufafanulia sehemu fulani ya dhamana hiyo ya kijamii katika Uislaam?

JAWABU: Dhamana ya kijamii katika Uislaam inatokana na shauku na mapenzi ya kibinadamu na kiutu tena ya kiwango cha juu kabisa kwa maana hiyo hakika Uislaam una anzia kwenye nukta ya utu au ubinadamu, na huitoa dhamana hii ikiafikiana na hali ya kibinadamu na kiutu na ikilenga kwenye upeo wake na katika nyanja zake za ubora  na kwa kusisitiza hilo historia haikuwahi kushuhudia kabla ya Uislaam  na historia  haikunukuu utamaduni wa aina yoyote baada ya Uislaam hadi hivi leo dhamana ya kijamii yenye kina kilicho sawa na kina cha dhamana ya kijamii katika  Uislaam.

 

MIFANO YA DHAMANA YA KIJAMII YA

KIISLAAM 

Hakika dhamana ya kijamii katika Uislaam inasema yafuatayo:

1- Hakika kila mtu anae kufa hali ya kuwa na madeni, au ameacha familia bila msimamizi na mtu wa kuitunza familia yake, ni juu ya Imam wa Waislaam kulipa madeni yake, kama ambavyo ni juu yake kuitunza na kuilea familia yake.

2-Kila anae fariki hali ya kuwa ana mali, mali yote ni ya warithi wake.

3- Pamoja na hayo, huduma za kimali ambazo hutolewa na Baitul mali ya Waislaam kwa kila mtu katika umma wa kiislaam, ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya mwanzo na kwa ajili ya kujipatia maisha mema.

Je unadhani-pamoja na yote hayo- unadhani kunadhamana kama hii ambayo imo ndani ya Uislaam, hata kama ni katika utamaduni ulio endelea na wenye kina kikubwa zaidi? Kwa hakika na bila shaka yoyote hakuna kitu kama hicho, bali ukweli ni kuwa mifumo mingine ya utawala ya kiulimwengu na ya kijahili iliyo kuwepo kabala ya Uislaam vilevile mifumo ya ulimwengu inayo dai kuwa imeendelea na iliyo kuwa na maendeleo ya kielimu na iliyo staarabika katika zama zetu hizi huwajibisha kutoa mapato makubwa kwenye urithi, kama ambavyo wao hawalipi deni la yeyote na wala hawabebi jukumu la kuitunza familia ya marehemu na hakuna shaka hapa kutaja  baadhi ya mifano ya kiislaam juu ya jambo hili.

 

MFANO WA KWANZA

Katika Nusuus (dalili) za kisheria za kiislaam, kuna dalili nyingi zinazo tilia mkazo juu ya haya tuliyo yataja  ya dhamana ya kijamii ya kiislaam na dalili hizo bila shaka zinatujulisha juu ya namna Uislaam unavyotilia mkazo na hima juu ya jamabo hili na katika upande huu wa kibinadamu na kijamii ulio mkubwa, kiasi kwamba imekaririwa kwa mara kadha zikinukuliwa dalili juu ya suala hilo kutoka kwa Mtume wa Uislaam (s.a.w) na maimam wa kizazi kitwaharifu cha Mtume (s.a.w).

Kwa mfano imepokelewa kutoka kwa Abi  Abdillah Jaafar bin Mohammad  As-swaadiq (a.s) Imam wa sita wa Ahlul bayti (a.s), ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema:

 (انا اولي بكل مؤمن من نفسه و علي (ع) اولي به من بعدي)

(Mimi ni bora kabisa au mwenye haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake na Ali (a.s) ni bora zidi na mwenye haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake baada yangu).

Akaulizwa:Nini maana ya maneno hayo?

Akasema: Kauli ya Mtume (s.a.w): (Mwenye kuacha deni, au familia basi ni juu yangu mambo hayo na mwenye kuacha mali basi ni ya warithi wake).[11]

 

MFANO WA PILI

 Ali bin Ibrahiim katika tafsiri yake ametoa hadithi, kwa sanadi yake iliyo tajwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) ya kuwa yeye alikuwa akisema: (Hakuna mdai yeyote alie kwenda na mdaiwa wake kwa  mtawala kati ya watawala wa kiislaam na ikabainika kwa yule walii ya kuwa ni tajiri na mwenye uwezo, isipokuwa humuokoa yule fakiri kutokana na deni lake, na deni hilo kuhamia kwenye dhima ya mtawala yule wa Waislaam kutokana na mali iliyoko mikononi mwake kati ya mali za Waislaam).[12] 

 Amesema Imam Swadiq (a.s) baada ya kunukuu hadithi hii kutoka kwa Mutme (s.a.w): (Na hakukuwa na sababu ya kusilimu Mayahudi wote isipokuwa baada ya kusikia kauli hii kutoka kwa Mtume (s.a.w) na kwamba wao walipata tumaini juu ya nafsi zao na juu ya familia zao.[13]

 

MFANO WA TATU

Shekh Mufiid (Quddisa sirruhu) ametoa hadithi katika kitabu chake Al-majaalis, kwa sanadi yake kutoka kwa Imam Abi Abdillah As-swadiq (a.s) ya kuwa alikuwa akisema: (Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alipanda kwenye Mimbari, vitukuta vyake vikabadilika na rangi yake kumeremeta, kisha akageuza uso wake na kusema: Enye waislaam! Hakika si jambo jingine mimi nimetumwa na kiama, kama vitu viwili hivi- hadi akasema- enyi watu! Mwenye kufariki na kuacha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake na mwenye kuacha deni au familia bila muangalizi, ni juu yangu na hurejeshwa kwangu)[14] 

Pia ametoa hadithi kutoka kwa Abi Abdillah As-swadiq (a.s) ya kuwa amesema: (Yeyote atakae kuwa na mali (yaani atakae chukua deni) kwa mtu fulani na hakuitumia mali hiyo vibaya (kwa israfu), au katika maasi, na ikamuwia vigumu kulipa deni hilo, ni juu ya mwenye mali kumpa muhula (muda) mpaka Mwenyezi Mungu amruzuku na aweze kulipa deni hilo na ikiwa Imam muadilifu yupo, ni juu yake kumlipia deni hilo, kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w): Yeyote atakae acha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake na mwenye kuacha deni au familia, ni langu na  ni juu yangu  na ni juu ya Imam kuchukua dhamana aliyo ichukua Mtume (s.a.w)).[15]

 

MFANO WA NNE

Hakika Uislaam- kwa ubora wa mfumo na nidhamu yake uliyo nayo ya Baytil mali ya Waislaam na dhamana ya kijamii ya kiislaam- imeufanya umma wa kiislaam kuwa tajiri na ufakiri katika dola hilo umekaribia kuwa sawa na khabari ya kana (khabari iliyo kuwa) kutokana na dola la kiislaam, ambalo lemeenea kila mahala, na lenye ardhi kubwa na pana na zilizo mbali, ardhi ambayo takariban zaidi ya tatu ya nne ya ardhi hiyo ni yenye kukaliwa na watu, na yenye wakazi wengi.

Ndio, hakika Shekh Hurrul Amiliy ametaja katika kitabu chake maarufu: (Wasaailu-shia) kisa kifuatacho akisema: Hakika Imam Amirul muuminiin Ali bin Abi Twalib (a.s) alikuwa akitembea katika mitaa na vichochoro vya mji wa Al-kufa, ghafla akamuona mtu mmoja akiomba watu misaada: akastaajabu sana kutokana na mtu huyo na akawageukia walio kuwa pembezoni mwake akijiuliza: Ni kitu gani hiki?

Akajibiwa: kuwa ni Mkiristo amezeeka na kuwa na umri mkubwa na hana tena uwezo wa kufanya kazi na hana mali ya kumuwezesha kuishi, kwa hivyo ndio maana anawanyooshea watu mkono kwa kuomba.

Imam (a.s) akasema hali ya kuwa ni mwenye ghadhabu: Mmemfanyisha kazi wakati akiwa kijana mpaka alipo fikia utu uzima na uzee mkamtelekeza na kumuacha?

Kisha Imam (a.s) akaamuru atengewe fungu yule Mkiristo katika baytul mali ya Waislaam litakalo mfanya aishi maadamu bado yuko hai.[16]

Hakika kisa hiki kinatufahamisha ya kuwa ufukara ulikaribia kutokuwa na nafasi katika dola la kiislaam, hadi ilifikia Imam Amirul muuminiin (a.s) akimuona fakiri mmoja  hushangaa na kustaajabu na kuliona tukio hilo kuwa ni tukio lisilo la kawaida na hali isiyo ya kawaida na halinasibiani na jamii ya kiislaam na dola au nidhamu ya kiislaam, kisha wakati huo akamuwekea fungu litakalo mfanya aishi maisha mazuri na yenye furaha pamoja na kuwa ni Mkiristo na hafuati dini ya kiislaam, na alifanya hivyo ili kusiwe katika nchi ya kiisalaam mfano au tukio moja linalo onyesha hali ya ufukara na kutokuwa na kitu  na ili ulimwengu ufahamu hali waliyo nayo Waislaam: Ya kuwa serikali ya kiislaam inampango wa kuangamiza janga la ufukara na kuinua hali ya  maisha ya mafakiri na masikini na si kwa mustawa wa Waislaam pekee yao, bali inaupiga vita ufukara hata kwa Makafiri  maadamu wako chini ya uangalizi wa dola la kiislaam.

 

MFANO WA TANO

Shekh Kulayni ametoa hadithi kwa sanadi yake iliyo tajwa kutoka kwa Hassan amesema: (Hakika Ali alipo washinda Twalha na Zubayri) katika vita vya Jamal na katika vita vyake alivyo pigana pamoja na wapingaji (Naakithiin) watu walirejea wakiwa wameshindwa, na wakampitia mwanamke mmoja alie kuwa mja mzito njiani, na alipo waona akashikwa na fazaa na mshutuko mkubwa na ikawa ni sababu ya kutoka kwa  kilicho kuwa tumboni mwake kikiwa hai na kutatizika hadi akafariki, kisha mama wa mtoto huyo nae kafariki baadae, Imam Ali (a.s) akampitia mama huyo yeye na maswahaba zake hali ya kuwa mama yule akiwa amelala chini na mwanae akiwa njiani, akawauliza kuhusiana na kilicho msibu mama huyo?

Wakasema: Hakika alikuwa ni mja mzito na akashikwa na fazaa na mshutuko wakati alipo ona mapigano na namna walivyo shindwa.

Akasema: Akawauliza: Ni yupi alifariki kabla ya mwengine? Akajibiwa: Hakika mwanae ndie alie fariki kabla ya mama.

Akasema: Imam (a.s) akamuita mumewe baba wa mtoto alie fariki akampa theluthi ya fidia kama urithi wa mwane, kisha akamrithisha mama yake theluthi nyingine ya fidia, kisha akamrithisha mume vilevile kutoka kwa mkewe nusu ya fidia ambayo aliirithi kutoka kwa mwanae na kuwarithisha jamaa au ndugu wa mke alie fariki fidia iliyo bakia, kisha akamrithisha mume pia katika fidia ya mkewe alie fariki nusu ya fidia nayo ni: Dirhamu elfu mbili na miatano na jamaa za mwanamke alie fariki akawarithisha nusu ya fidia nayo ni:Dirhamu elfu mbili na mia tano na alimpa kiasi hicho kutokana na kutokuwa na motto mwingine tofauti na yule alie toka kutokana na fazaa iliyo mshika.

Akasema: Na Imam (a.s) alitoa mali yote hiyo kwenye Baytul mali ya Basrah.[17]

Ndio, hivi ndivyo Uislaam ulivyo weka Baytul mali ya Waislaam kwa ajili ya manufaa ya Umma na kutatua matatizo yao na kuwapa haki zao, kwani-kama ilivyo pokelewa katika hadithi tukufu- (Haki ya muislaam haipotei)na katika hadithi nyingine imepokewa ikisema (Damu ya Muislaam haimwagiki bure)[18] na kwa dalili hizo Uislaam ukauwekea Umma wa kiisalaam mahitaji yenye kumtosheleza kupitia mpango wake wa dhamana yake ya kijamii yenye uadilifu.

 

UISLAAM NA JESHI

SWALI: Je katika Uislaam kuna jeshi maalum lililo pangwa na lenye nidham maalum?

JAWABU: Ndio na lenye nidhamu iliyo bora kabisa na lililo pangwa katika sura iliyo bora kabisa.

SWALI: Je katika Uislaam kuna sheria ya kujiunga na jeshi kwa lazima bila ya hiari?

JAWABU: Hapana, kujiunga na jeshi katika Uislaam ni suala la hiari.[19]

SWALI: Basi inakuwa vipi  kujiunga kwake na uandaaji wa jeshi? 

JAWABU: Hakika dola au serikali ya kiislaam  huandaa sehemu kubwa na mahala maalum nje ya miji, iliyo andaliwa kwa aina tofauti za silaha na kuwahiarisha watu kwenda kushiriki katika mazoezi ya kijeshi katika sehemu hizo  katika nyakati zao za faragha  kama siku ya Ijumaa na ziku zinginezo ambazo hawako kazini, bila ya kutofautisha kati ya yeyote atakae kushiriki, wakubwa kwa wadogo.[20]

Na kwa njia hii takriban watu wote hushiriki katika hufanya mazoezi na kuiondolea serikali matumizi ambayo inge yatoa kwa ajili ya jeshi, kama ambavyo wafanya kazi hubakia makazini na kwenye familia zao, kwa hivyo kila mtu hufanya mazoezi kila siku-kwa muda wa saa moja au masaa mawili, kwa mfano-kisha kurudi kwenye kazi yake na kubakia na  familia yake.

Na pindi adui anapo ivamia nchi au dola inakuwa ni wajibu kwa wote kupigana  kwa kuutetea Uislaam na mwenye kupendezewa kulitumikia dola na serikali kwa hiari yake, hupangiwa mshahara maalum, ili abakie wakati wote na bila kusimama akiwa ni mhudumu wa dola la kiislaam.

 

VIFAA VYA KIVITA

SWALI: Ni upi mtizamo wa kiislaam kuhusiana na vifaa vya kisasa vya kivita?

JAWABU:Mtazamo wa kiislaam ni kuwa niwajibu kutengeneza na kuwa na vifaa vitakavyo liwezesha dola au serikali ya kiislaam kujibu mashambulizi na kujilinda na kulinda heshima ya Uislaam na amani ya waislaam[21] na hilo linatokana na kauli yake Mwenyezi Mungu:

(وأعد وا لهم ما استطعتم من قوة)[22]

(Na waandalieni nguvu kwa kadri ya uwezo wenu)

SWALI: Dola au serikali huwa na mipango gani kuhusiana na familia za wanajeshi wanao kufa vitani?

JAWABU: Ikiwa familia  hiyo ni mafukara na wasio jiweza, hupewa kiwango cha kutosheleza mahitaji yao  kulingana na hadhi yake na kama familia hiyo haikuwa hivyo, haipewi kitu isipokuwa ikiwa katika kuwapa chochote kuna maslaha na mfano wa hayo.

SWALI: Ni upi msimamo wa Uislaam kuhusiana na amani na vita?

 JAWABU: Uislaam ni dini ya amani na utulivu kama alivyo sema Mwenyezi Mungu alie tukaka:

يا أيها الذ ين آمنوا أد خلوا في السلم كافة [23]       

(Enyi mlio amini ingieni kwenye Uislaam wote) na Uislaam hufanya kazi ya kueneza amani  na usalama  ulimwenguni na huenda mbio kuzima chochoko ya vita na kuzima moto wake wenye kulindima na kung’oa mizizi ya chanzo chake kati ya watu, kwa kung’oa vyanzo na sababu zipelekeazo kutokea kwa vita  na badala yake kuweka vyanzo vinavyo chochea mapenzi na kuelewana na vinavyo chochea kuwepo sulhu na utulivu na kuacha kabisa suala la vita na kuwa na utulivu hata kama adui atakuwa anafanya hadaa na kutoa wito wa kutaka kuwepo amani, amesema Mwenyezi Mungu alie takasika:     [24] وإن جنحوا للسلم فاجنح لها

(Na ikiwa wataelekea na kumili kwenye amani basi nanyi elekeeni  kwenye amani).

Na wakati huo huo Uislaam unaharamisha mambo ya kutumia nguvu na vitisho na mauaji ya kuvizia au mauji ya kawaida na inapiga vita kila jambo lipelekealo kuwa na khofu na kuogopa na wasiwasi na kutokuwa na utulivu kati ya watu.

 

UHURU KATIKA UISLAAM

SWALI: Je kuna uhuru katika Uislaam?

JAWABU: Ndio, tena uhuru ulio bora kabisa kati ya migawanyo ya uhuru, na ambao ulimwengu hauja wahi kuufikiria wala kuuotea katika utamaduni wa juu kabisa kati ya tamaduni za hapa ardhini.

SWALI: Ni upi uhuru wa kiislaam?

JAWABU: Uhuru wa kiislaam ni wa aina nyingi, na hapa tutataja baadhi tu kati ya aina hizo za uhuru huo kama ifuatavyo:

  

UHURU WA BIASHARA NA UCHUUZI

 1-Uhuru wa kufanya kazi na kufanya Biashara, kila mtu kati ya watu wa Umma wa kiislaam anayo haki ya kujichagulia kazi au shughuli aitakayo kuifanya kwa ajili ya uchuuzi au kuwa ndio chanzo cha mapato yake, kwa hivyo akichagua uwindaji ni juu yake, au kuchimba madini na ngawira zilizoko ardhini, au kukusanya mambo ya mubaha na kuyamiliki na mengineyo kati ya vyanzo halali vya uchuuzi, kama ambavyo ni ni haki ya mfanya biashara kuingiza nchini bidhaa azitakazo au kusafirisha nje ya nchi bidhaa azitakazo, au kununua na kuuza bidhaa azitakazo, katika upande huo kahakuna kizuizi kamwe, katika Uislaam hakuna ushuru (Tax) wala hakuna Leseni ya biashara wala sharti, ndio hushurutishwa bidhaa zisiwe  za haramu-kama mvinyo-(vileo) na kusiwe na riba katika biashara hiyo au isiwe ni biashara ya haramu na mfanya biasha asifiche bidhaa wakati wa mahitaji kwa ajili ya kusubiri msimu ambao kutakuwa na uhaba wa bidhaa hizo na katika biasha hiyo kusiwe na madhara kwa watu na katika uchumi wao.

 

UHURU WA VIWANDA NA UKULIMA

2-Uhuru katika kilimo na viwanda, kwa maana mwenye kutaka kujishughulisha na kilimo kiasi chochote cha ardhi akitakacho na kwa aina yoyote ile aitakayo, anayo haki ya kufanya hivyo  na wala hakuna katika Uislaam kitu kiitwacho ( kilimo cha kisasa) mpango ulio ingizwa kutoka katika nchi zisizo za kiislaam, ndio ardhi hiyo ikiwa ni ardhi iliyo (kombolewa kwa nguvu) ni wajibu kwa mkulima kutoa malipo ya ukodishaji wa ardhi hiyo-kwa kiasi kidogo sana-na kuilipa serikali au dola na hiyo ndio iitwayo kwajina la (kodi) ya ardhi, na  mkulima ikiwa ni fakiri ni wajibu kwa serikali kumkidhia haja yake kulingana na hadhi au hali yake na hakuna kizuizi cha mtu kulima kiasi chochote cha ardhi akitakacho kwa sharti kwamba asiwanyime wengine nafasi na fursa ya kulima na alime mazao yoyote ayatakayo isipokuwa yatakayo kuwa na madhara kama na serikali haina haki kuchukua mapato isipokuwa (Khumsi) na (Zaka) pamoja na kuchunga masharti yake kama tulivyo eleza hapo kabla, na vilevile viwanda vyote, viko huru- kwa maana kamili ya uhuru-isipokuwa katika vitu vilivyo haramu katika Uislaam kama viwanda vya pombe (Vileo) na madawa ya kulevya.

 

UHURU WA UJENZI NA UENDELEZAJI WA MIJI   

3-Uhuru wa ujenzi na uendelezaji wa ujenzi wa nchi na miji, mwenye kutaka kuiendeleza ardhi kwa namna yoyote ile iwayo, anayo haki ya kufanya hivyo,  kwa hivyo basi mtu yeyote chini ya kivuli cha serikali ya kiislaam anayo haki ya kujitengea ardhi ya halali na kujenga akitakacho kwenye ardhi hiyo kama nyumba au sehemu ya kibiashara, au kiwanda, msikiti, Husainiyya, Madrasa, Dispensari, Hospitali, au mfano wa havyo kwa uhuru kamili na katika ujenzi na uendelezaji hakuna kabisa kitu kiitwacho Leseni  na serikali au dola halina haki kuchukua chochote kwa mtu huyo walau senti moja  kwa ajili ya ardhi au kinginecho, hakika Uislaam umeweka kanuni isemayo kuwa (Mwenye kuhuisha ardhi zilizo kufa  yaani zilizo telekezwa basi ardhi hiyo ni milki yake)[25] isipokuwa ardhi hiyo ikiwa  (imekombolewa  kwa nguvu) wakati huo ni juu ya mwenye kuiendeleze ardhi hiyo kutoa malipo ya ukodishaji kwa serikali.

Na ikiwa hukumu hii itatekelezwa  katika ardhi na uendelezaji wa ardhi basi itakuwa inatosheleza kukidhi haja za watu katika suala la makazi, na kutoweka tatizo la makazi lililo enea katika nchi zote za kiislaam.

 

UHURU WA MTU  KUISHI NA KUSAFIRI MAHALA 

APATAKAPO

4-Uhuru wa kusafiri na kuishi,  yaani mwenye kutaka kuishi mahala fulani, au kusafiri mahali fulani anahiari ya kufanya hivyo bila sharti wala kikwazo,  katika Uislaam hakuna mipaka ya mahala, wala vikwazo vya kijinsia wala ubaguzi wa kirangi, lugha na kwa uhuru huu suala la uraia na jinsia na suala la pasport za kusafiria huporomoka na mengine yote yanayo ambatana na hayo, kama ambavyo nchi nyingi za ulaya zilivyo andoa vitu hivyo na kupinga bidaa hii yenye kuwaudhi na kuwakera wananchi wake na nchi zao.

 

UHURU WA NASHATI ZA KIJAMII NA KISIASA

5-Uhuru wa kutoa huduma za kijamii au kuihudumia jamii na harakati za kisiasa bila kuwa na vikwazo,-isipokuwa harakati zilizo haramishwa na Uislaam nazo ni chache sana, kwa maana hiyo hakuna idara ya upelelezi kamwe, kwani haijuzu kumfanyia yeyote upelelezi au tajassusi, kwa hivyo katika Uislaam hakuna wizara ibebayo jina la Wizara ya upelelezi na mfano wa hayo, isipokuwa wizara ya kukusanya habari (Wizara ya habari) kwa ajili ya maslahi ya Umma na kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi  na usalama wake, kwa hivyo katika dola la kiisalaam[26] kila mtu yuko huru kuandika na kubainisha ayatakayo na katika maneno yake na auandishi wake wa vitabu na yuko huru kuunda vikundi mbali mbali vya kijamii na jumuia na vikundi vya ushirika na vikundi vya kheri na kukusanya misaada mbali mbali na vitu vya kujitolea na kutoa au kuchapisha majarida mbali mabli na magazeti na kuanzisha redio na televisheni na visivyo kuwa hivyo.   

  

UHURU WA HARAKATI NA NASHATI  ZINGINEZO

6- Uhuru wa nashati zingine za mtu mmoja mmoja au za kijamii, kwa mfano: kila mtu mwenye kufahamu udreva, yuko huru kuendesha bila ya haja ya kumpatia leseni au mfano wake, kama ambavyo maiti hahitajii ruhusa ili aandaliwe na  kuzikwa, bali ni juu ya jamaa zake kusimamia suala la kumuandaa na kumzika sehemu yoyote waitakayo au sehemu aliyo iusia yeye mwenyewe marehemu, bila ya haja ya kutoa kodi au Risiti au mfano wa hayo na hukumu ni hiyo hiyo katika mambo mengine.

SWALI: Kutokana na mliyo yataja itapelekea kufungwa kwa ofisi na idara nyingi?

JAWABU: Ndio…na hivyo ndivyo dola la kiislaam lilivyo kuwa, halikuwa na idara isipokuwa chache sana  na kwa maana hiyo ndio maana tukasema-hapo kabla-ya kuwa wafanya kazi katika dola au serikali ya kiislaam ni wachache sana, na ni wachache kupita kiasi na kwa sababu ya uchache wa wafanya kazi majukumu ya serikali na mzigo wa serikali na dola la kiislaam utapungua na wala muundo wa serikali au dola hauta  beba mzigo wa matumizi mengi ya pesa (yaani dola halita tumia pesa nyingi katika bajeti yake).

 

UTOAJI WA HUKUMU NDANI YA UISLAAM

SWALI: Je katika Uislaam kuna hakimu na utoaji wa hukumu? 

JAWABU: Ndio, katika Uislaam kuna aina nzuri sana ya utoaji hukumu na kuna mahakimu walio waadilifu zaidi.

SWALI: Hakimu na utoaji wa hukumu huwa vipi katika Uislaam?

JAWABU: Katika Uislaam Hakim ni wajibu au ni lazima awe ni muumini na muadilifu, mwenye elimu ya utoaji hukumu  na awe ni Mujtahidi katika mas’ala ya utoaji hukumu na katika hukumu zake na utoaji hukumu ni wajibu uwe kwa kutegemea dalili na viapo, bila kuwa na vikwazo katika mahakama wala kusiwe na mizunguko na bila ya kuwepo ufunguzi wa mafaili wala stakabadhi wala ulipaji wa malipo kamwe na hakuna haja ya kutanguliza ufunguaji wa faili la mashtaka  na mfano wa hayo kama mafaili ya mashtaka yatumikayo katika zama hizi kwenye mahakama mbalimbali na katika utoaji wa hukumu. 

Na kwa ajili ya urahisishaji, uadilifu huu uliopo kwenye mahakama za kiislaam na kutoa egemea au kumili sehemu fulani kuliko shurutishwa kwa Hakimu katika Uislaam, Hakimu au Kaadhi mmoja anaweza kusikiliza madai ya pande zote mbili mshitaki na mshitakiwa na kutoa hukumu kwa haraka sana iwezekanavyo na hilo hufanyika juu ya vipimo na misingi ya Uislaam na ushahidi wa mashahidi walio waadilifu na kutokana na hali hiyo ndio maana Kaadhi mmoja alikuwa akihukumu mji mmoja wenye (Mamilioni) ya watu  kiasi kwamba hakuna tatizo lolote libakialo linalo husiana na mambo ya mahakama au utoaji hukumu kamwe.

SWALI: Hakimu hupata wapi riziki yake kwa kazi aifanyayo?

JAWBU: Hupata riziki yake kutoka kwenye Baytul mali.

SWALI: Ni ipi kazi ya Kaadhi (Hakimu)?

JAWABU: Kadhi kwa kusaidiwa na wasaidizi wake hufanya kazi zifanywazo na ofisi au idara nyingi katika serikali tawala, katika zama hizi, hakika yeye husimamia mambo ya waqfu na kuwasimamia watumishi wa waqfu hizo na hukusanya mali ya  watoto wadogo na kuiihifadhi ili baadae awape wenyewe pindi masharti yanapo kamilika na huizuia mali ya punguwani na kufungisha ndoa na kutoa au  kusimamia suala la talaka na huuza na kununua na kuwekesha reheni na kukodisha  na kutatua mizozo kati ya watu na kutekeleza hududi za kisheria kati yao na mengineyo.[27]

 

UWAKILI KATIKA UISLAAM

SWALI: Je katika Uislaam kuna mfumo wa mawakili, kwa namna hii ijulikanayo katika mahakama za kisasa?

JAWABU: Katika Uislaam hakuna mfumo wa uwakili kwa namna hii iliyopo hivi sasa na wala Uislaam hauhitaji idadi hii kubwa ya mawakili, kwani mambo yote na hasa mambo ya mahakama na utoaji hukumu katika dola la kiislaam huendeshwa kwa njia nyepesi na kwa urahisi sana tena kwa amani na uaminifu.

SWALI: Uislaam huwafanyisha nini au huwatumikisha vipi mawakili na wafanyakazi ambao dola la kiislaam haliwatambui kutokana na kazi zao, ikiwa utashika hatamu ya uongozi na kuendesha serikali?

JAWABU: Hakika Uislaam hauushutukizi umma au watu kwa mabadiliko au marekebisho ya ghafla bali katika kufanya mabadiliko na marekebisho huwa nao sambamba na kwa njia ya taratibu, kwanza kabisa wale ambao haizitambui kazi  zao huwaandalia kazi zinazo wiana na hadhi au utaalamu wao au zinazo nasibiana nao, kisha kuwalipa kutoka kwenye hazina ya dola au serikali kiwango kitakacho weza kuwasaidia  katika mambo yao ya kimaisha, mpaka ifikie kupata kazi ambazo wao wenyewe wanataka kuzifanya, je  baada ya hatua hizi kuna yeyote kati ya wale  ambao serikali haizitambui na kuzikiri  kazi zao  atakae chukua hatua yeye mwenyewe na kuitilia mgomo serikali ya kiislaam baada ya kuwa serikali ya kiislaa imemuandalia kazi inayo nasibiana na utaalamu wake au nafasi yake  kati ya kazi zilizo huru na zenye manufaa na kumsaidia mpaka akawa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa fakhari na kwa raha mustarehe bila ya kukereka?

Na vilevile Uislaam hufunga kabisa sehemu ziuzazo pombe kama Mabaa na majumba ya ufuska na mfano wa hayo pamoja na kutilia mkazo kwa kiwango kikubwa mambo ya maisha yao na kuanzisha vituo au kazi zinazo wiana na sehemu na hadhi zao kama kazi ambazo zitawafanya wapate riziki zao za halali na kuwazuwia kazi hizo kufanya matendo ya haramu.

 

SWIHHA NA AFYA KATIKA UISLAAM

SWALI: Je katika Uislaam kuna nidham na mfumo wa mambo ya kiafya?

JAWABU: Ndio na mfumo ulio bora kabisa kuliko mifumo na nidhamu iliyopo ya kinga na utibabu, na inamifumo iliyo makini zaidi na mipana na yenye kuhusika na nyanja zote, kwa mfano inayo mifumo inayo husu afya ya mwili, roho na afya ya mtu mmoja mmoja na jamii na mifumo ya usalama wa hali ya hewa  anga na mazingira.

SWALI: Mfumo wa kiislaa wa kiafya  uko vipi?

JAWABU: Uislaam huweka jedwari kwa sura ya ujumla linalo husiana na afya ya ujumla kwa kuweka kanuni ya mambo matatu:

1-Kanuni ya kinga: Hakika kanuni hii hulinda na kumhifadhi mtu mmoja mmoja, Jamii na Mazingira ili yasienewe na maradhi ya kuambukiza au kuhamia kwa watu wengine na kinga hiyo hutimia kwa mambo yafuatayo:

(a): Kuharamisha vitu ambavyo ni sababu ya kuzuka kwa maradhi  na uambukizaji., kwa mfano: Pombe, madawa ya kulevya, uzinifu, kulawitiana, kusagana kati ya wanawake, mambo yenye madhara, miziki na mambo yasababishayo kero na Mabaa (sehemu za kuuza vileo) na madanguro (majumba ya ufuska) na vikao ambavyo watu hukaa uchi (yaani sehemu za shoo ambapo wanawake hukaa uchi) na mfano wa hayo.

(b) Kwa kuweka kanuni ya mambo na adabu  kumi za sunna zenye kumuelekea mtu mmoja mmoja na jamii, kama kanuni ya Usafi, Kuoga, Kutoa damu kwa ajili ya kusafisha mwili (Hijaama) na kutoa damu katika baadhi ya mishipa kwa kuchanja (Al-fasdi), kufunga, Kujipaka mafuta, Kuoa, kutumia tiba ya kunusa dawa, kutumia wanja, na kutumia (Nura) dawa ya asili kwa kujisafishia, namna ya kula na kunywa na namna ya kuvaa, sehemu ya kuishi, kulala, kuamka, na mengiyo.

     2-Tiba: Na hutimu hilo kwa kuelekeza baadhi ya madawa ya miti shamba na vyakula vyenye manufaa na vinavyo saidia katika kutibu magonjwa na yote hayo hufanyika kwa njia ya kawaida na nyepesi  na njia hii japokuwa haienei na kuyahusu magonjwa yote, isipokuwa ukweli ni kuwa hufukuza marahi na hasa yanapo kuwa yana anza, kama ilivyo elezwa  katika kitabu (Twibbun-nabiiy) (s.a.w) na katika kitabu (Twibbul-aimmah) (a.s) na mfano wa hayo.

     3-Kuchukua tahadhari: Hakika Uislaam huchukua tahadhari na kulinda suala la usafi wa mazingira na hufuatilia suala la usafi wa mazingira kutokana na kuchafuliwa na hufuatilia kwa makini afya ya kila mtu na kumlinda asipatwe na magonjwa ya kuambukiza, kama ambavyo  huwachunga matabibu na madaktari kwa makini kabisa na kuwajaza ndani ya nyoyo zao hali ya kiutu na dhamira safi na khofu ya Mwenyezi Mungu na kuwaadhibu pindi wanapo kiuka maadili, kwani utakuwa imefikia kuweka kanuni isemayo (Tabibu au Daktari ni mwenye dhamana hata kama ni hodari na mwenye uhakika na kazi yake) kitu ambacho humfunga na kumtia dhamana Daktari asiweze kupuuzia katika kumuangalia mgonjwa au kupuuzia katika kutoa matibabu, au kuto sema ukweli, bali kanuni hiyo inamfanya awe na hali ya umakini na umadhubuti wa hali ya juu kabisa na tahadhari kubwa  na mwenye kujichunga sana katika kumuandikia mgonjwa dawa na katika kuyafanyia uchunguzi maradhi na kuyatibu kwake  maradhi hayo. 

 

UISLAAM NA TIBA YA KISASA

SWALI: Je si kweli kwamba tiba ya kisasa imepata maendeleo makubwa na yenye kushuhudiwa ulimwenguni?
JAWABU: Hakuna shaka yoyote juu ya maendeleo yaliyo patikana katika tiba ya kisasa lakini ile misingi ambayo tumeitaja na ambayo ndio nguzo na vizingiti vya msingi na sababu za kiafya na swiha, misingi hiyo imevunjwa na kubomolewa, kwa maana hiyo ndio maana tunakuta kwamba maradhi yamekuwa yakiwashambulia wanadamu kwa njia za ajabu sana na kwa sura ya kushangaza, hata imefikia wingi wote huu wa madaktari na maduka ya madawa na mahospitali na mfano wa hivyo, havitoshelezi kurejesha hali nzuri ya kiafya duniani kwa sura ya ujumla.
Na kwa msingi huo bado tuna wakumbuka mababu zetu na mababa zetu ambao-kwa kuchunga na kulinda kwao nidhamu ya kiislaam katika mambo ya kiafya-wakiishi raha mustarehe na wakiwa na afya kamili na swiha nzuri na wakiwa na nguvu zao timamu mpaka wanapo fikia hatua ya kufariki, wakati ambapo tunaona katika zama zetu hizi ya kuwa kila nyumba haikosi kuwa na mgonjwa au maradhi na watu wengi utakuta kuwa wamekumbwa na ugonjwa au magonjwa ya aina tofauti.
SWALI: Sasa ni ipi njia ya kurekebisha na kutibu hali hii?
JAWABU: Njia ya kurekebisha na kutibu hali hii ni kufanya kila njia na kwenda mbio kurudisha ile mipango na ratiba na kanuni za ujumla za kiafya zilizomo katika Uislaam na kuzifanyisha kazi au kuzitekeleza katika jamii zetu na kuchukua tiba ya kisasa yenye manufaa na mambo mapya yaliyo gunduliwa katika tiba ya kisasa na kutoa mambo ya haramu na mambo yenye madhara katika tiba hiyo na kufungua njia na milango ya kufaidika na tiba ya miti shamba au tiba ya kizamani (kama waiitavyo wataalamu wa kisasa) na ambayo ni mujarrabu, ili zichanganyike tiba hizo mbili tiba ya zamani (yaani ya miti shamba) na tiba ya kisasa na kwa kufanya hivyo wanadamu na viumbe waweze kuokoka na kuepukana na maraadhi au magonjwa pia mabalaa na majanga ya kibina damu chini ya kigezo cha maradhi ya kushutukiza na kuua kwa ghafla.

 

UTAMADUNI WA KIISLAAM

SWALI: Je katika Uislaam kuna mifumo ya tamaduni za aina mbamlimbli?
JAWABU: Ndio, katika Uislaam kuna mifumo iliyo bora kabisa ya kitamaduni.
SWALI:Ni ipi mifumo hiyo?
JAWABU: Hakika Uislaam umefaradhisha na kuwajibisha suala la kutafuta elimu kwa mwanamke na mwanamume na ukaitambulisha elimu ambayo ni wajibu kwa watu kuitafuta katika makundi matatu:
1-Elimu ya Usulud-dini (Misingi ya dini) na elimu ya Furuud-dini na elimu ya Akhkaq (maadili) na adabu za kiisalaam na ikahimizwa kutafuta elimu zingine, na ikakuhesabu kufanya hivyo kuwa ni fadhila kwa mwanadamu na sharafu kubwa kwake, na ukahimiza na kusisitiza kuitekeleza elimu hiyo kwa matendo na kuandaa nyenzo na ukailazimisha serikali kutoa usaidizi katika utekelezaji wa yoye hayo.
SWALI: Hakika yote mliyo yataja yanawalazimisha wawe na maendeleo na wawe wamefikia hatua ya juu kabisa katika maendeleo, sasa kwa nini wamekuwa nyuma kimaendeleo?
JAWABU: Hakika Waislam wamechelewa na kuto endelea tangu wakati ambapo Uislaam ulipo achwa kutekelezwa ulimwenguni na tangu walipo acha na kuuweka kando mfumo wa kiisalaam katika mambo ya kiutamaduni, ama wakati walipo kuwa wameshika hatamu ya utamaduni wa kiislam na wenye kuutekeleza Uislaam, hakika wakati huo utamaduni wao uliupituka utamaduni wa kimagharibi wa hivi leo na hakuna dalili bora kabisa ya hilo kuliko wamagharibi kukiri wao wenyewe juu ya suala hilo, kwa mfano ukiangalia kiwango cha vitabu vyao maktaba zao shule zao na wataalamu wao, pamoja na ukiangali nyenzo walizo kuwa wakizitumia katika zama hizo, ni vingi sana ukilinganisha na vitabu, maktaba, shule, na wataalamu katika zama hizi pamoja na kuwa kuna maendelea katika nyenzo na sababu za kuyatekeleza hayo.

 

NYENZO ZA KISASA ZA KUELIMISHA WATU

SWALI: Ni upi msimamo wa kiisalaam kuhusiana na vyombo vya kisasa vya kuwaelimisha watu na kwa ibara nyingine: je Uislaam unaharamisha mashule, vyuo, Magazeti, majarida, televitioni, Redio, Sinema, na Satalaiti, Internet na mfano wa hayo?
JAWABU: Hakika Uislaam husisitiza na kuhimiza kila kinacho saidia au kuchangia kwa njia moja au nyingine kuwaelimisha watu na kueneza tamaduni za kibinadamu katika Umma, ndio, hakika Uislaam unaharamisha ufisadi na vyombo vyenye kusababisha uharibifu kati ya nyenzo hizi za kisasa, kwa hivyo ikiwa vitasafishwa na kuepukana na ufisadi basi Uislaam uko msitari wa mbele kabisa katika kuvikubali na kuzipokea nyenzo hizo.
SWALI: Ni ipi tofauti ya ujulma kati ya mfumo wa kiisalam wa kitamaduni na kati ya mfumo wa kitamaduni wa kimagharibi katika siku hizi?
JAWABU: Tofauti ya msingi ni kuwa: Uislaam umechanganya kati ya elimu na imani na utamaduni na Maadili na fadhila (ubora), wakati ambapo utamaduni wa kimagharibi kwa hivi leo hauna kitu kiitwacho imani, maadili na fadhila, na kwa kufuatia suala hilo elimu mbayo ndio wasila na nyenzo bora kabisa ya kukuza utamaduni na kuleta maendeleo vitu ambavyo ndio nyenzo yenye nguvu zaidi ya kuleta maelewano na kufahamiana na amani na usalama katika umma, bali katika ulimwengu wote imekuwa ndio nyenzo ya kuwafanya watu wamomonyoke kimaadili na kutengana na kimekuwa chombo cha kusabibisha khofu, fazaa, fujo na kutokuwa na utulivu na vita na uharibifu katika umma, bali katika ulimwengu wote.

 

AMANI KATIKA UISLAAM

SWALI: Je Uislaam ni dini ya vita, au ni dini ya amani?

JAWABU: Uislaam ni dini ya amani, Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:

[28]يا أيها الذ ين آمنوا اد خلوا في السلم كافة

Enyi mlio amini ingieni katika Uislaam wote. 1 Ama ikiwa mtu mmoja  atamshambulia mtu fulani, au akaanzisha vita na kuwapiga vita Waislaam, wakati huo Uislaam haukai kimia na kusimama ukiwa una agaalia tu bila kufanya chochote, bali unajibu mashambulizi na kujitetea kwa ajili ya kuhakikisha uadilifu unapatikana na ukweli unakuwepo na kuzuwia uadui na kuondoa dhuluma itakayo kuwa ikifanywa.

SWALI: Uislaam unaihami vipi amani?

JAWABU: Uislaam unaona ya kuwa kuna wajibu wa kuenea na kutawala Amani ndani ya nchi na nje ya nchi, ama kuhusiana na ndani ya nchi huzuia kufanyika kwa maovu na nje ya nchi haifanyi uchokozi kwa nchi yeyote au mtu yeyote na hutoa kipigo kwa wale wachokozi na wenye kuvuka mipaka ya nchi.

SWALI: Uislaam unapinga vipi maovu?

JAWABU: Uislaam unapinga maovu na maasi kuanzia kwenye mizizi yake na kutibu sababu zake, kwani sababu za maovu ni kama zifuatazo: Ufukura, Mambo yasabaishayo ufisadi, Ujinga, Uadui, Matatizo, na mfano wa hayo na Uislaam unayapiga vita mpaka uhakikishe umeyaondoa kabisa, na mambo hayo yanapo toweka, maovu yatapungua yenyewe.

Kwa hivyo basi kutokana na ubora wa mifumo ya Uiislaam iliyo madhubuti na mipango yake iliyo salama, inauwezo wa kutokomeza ufukara na kuwatajirisha mafukara au kuwafanya wasiwe wahitaji na kuwajulisha watu madhara ya ufisadi wa kijinsia na ufisadi wa kunywa pombe, kwa kupambika na tabia ya kanaa’a (kutosheka na unacho kipata) hujizuia na mambo ya kifahari na kunywa pombe na kueneza elimu na utamaduni na kuteketeza kabisa sababu za uadui na chuki na kutatua matatizo kwa njia nyepesi na utoaji hukumu wa haraka, kwa kufanya hivyo unaweza kung’oa mizizi ya maovu na kupandikiza mbegu za mapenzi na maelewano na umoja na amani kati ya umma na katika ulimwengu wote.

 

UFUATILIAJI  WA WAHALIFU NA KUWAADHIBU

SWALI: Anae fanya uhalifu katika Uislaam huadhibiwa vipi?

JAWABU: Hakika Uislaam-baada ya kuandaa mazingira mazuri na kuteketeza sababu za uhalifu katika jamii-wakati huo inaweka adhabu kwa mhalifu na mwenye kufanya maovu, kwa sababu atakuwa amefanya maovu na uhalifu huo kutokana na uchafu wake mwenyewe wa kimaadili na kupotoka kwake kimaadili na kutokana na upotovu wake na uadui wake kwa jamii yake na wananchi wenzake ambao ni waaminifu, hakika muhalifu wakati huo atakuwa ameitia doa na kuharibu sifa ya jamii yake na kuvunja Usalama na Amani ya jamii na anakuwa amewapora utulivu wao kwa hiyo huadhibiwa kwa adhabu kali, na adhabu hiyo hutekelezwa kwa haraka sana, na Uislaam wakati huo hulisafisha anga ili matendo maovu  kama hayo yasiweze kukaririka katika jamii.

Kutokana na haya inabainika wazi kabisa kuwa Uislaam hauruhusu kutekeleza  kanuni za kuwajazi wahalifu peke yake na kuzitekeleza bila ya hukumu zingine, kama ilivyo zoeleka katika zama hizi katika baadhi ya nchi za kiisalaam, na Uislaam huliona kuwa tendo kama hilo lenyewe ni uhalifu dhidi ya Uislaam, kwa sababu ndani yake kuna udhalilishaji wa Uislaam wenyewe na heshima yake na heba yake na kushikamana na tuhuma na sababu za kuwa Uislaam ni dini ya nguvu na ugumu kwa wananchi si dini yenye huruma na iliyo laini katika hukumu zake.

 

ADHABU YA KIFUNGO JELA

SWALI: Uislaam huzifanyia nini jela?

JAWABU: Hakika Uislaam unaona ya kuwa kanuni zilizo wekwa na wanadamu na zitumikazo kwenye nchi mbali mbali hazina maana na kima chochote kamwe bali kanuni iliyo bora na yenye maana ni kanuni iliyo telemka kutoka mbinguni au kanuni ya Mwenyezi Mungu tu na kwa msingi huu makosa mengi na uhalifu mwingi  wa kikanuni katika zama hizi si makosa wala uhalifu katika mtizamo wa kiisalaam, mpaka ifikie hatua ya kumtia jela mwenye kukiuka kanuni hizo, ama uhalifu na makosa yanayo zingatiwa na Uislaam kuwa ni makosa na ni uhalifu, kama Wizi, Uzinifu, Uislaam umekwisha ainisha na kubainisha adhabu kali na ya haraka dhidi ya makosa hayo na si kufungwa jela, ndio kuna makosa na uhalifu mdogo ambao Uislaam umeyawekea adhabu ya kukaa jela-kama mtu mwenye uweze (tajili) anae zembea na hataki kulipa deni lake-na Jela katika Uislaam ni ibara ya kuwa Kaadhi wa kiislaam humkabidhi muovu na mhalifu anae stahili kukaa jela kwa mtu fulani ili amzuwie na kumfungia katika chumba cha nyumba yake-kwa mfano-na kwa maana hiyo katika Uislaam hakuna jela kwa maana na mafhumu yajulikanayo katika zama hizi na yaliyo enea katika nchi za kiislaam kamwe na unapo lazimika kujenga jela, ujenzi huo unakuwa ni ujenzi wa jela ya kawaida, (si kama jela tuzionazo katika nchi za kimagharibi), kwa hakika jela hizo zina kuwa ni shule za malezi kwa wahalifu na sehemu ya  kuwaelimisha kwa kuwafundisha tamaduni na elimu za kibinadamu  zilizo sahihi.

 

AMANI  KWA WOTE

SWALI: Uislaam unaweza vipi kuhifadhi na kulinda amani nje ya dola la kiisilaam na kwa watu wote?

JAWABU: Hakika Uislaam haufanyi uchokozi kwa yeyote kamwe na wala hauvuki mipaka na kufanya uadui na uchokozi kwa dola au nchi yoyote, na dola lolote au nchi yoyote inapo taka Amani kati yake na dola la kiislaam, Uislaam nao humili kwenye amani hiyo, Mwenyezi Mungu alie takasika amesema:

[29]وان جنحوا للسلم فاجنح لها

(Na ikiwa watamili kwenye Amani basi nayi elekeni kwanye amani hoyo).  Na dola la kiislaam linapo fanyiwa uchokozi na kushambuliwa, Uislaam unasimama na kujitetea  na kuutetea umma kwa sura iliyo bora kabisa ambayo historia haija wahi kuona mfano wake, na dola lolote linapo fanya uchokozi juu ya dola la kiislaam au nchi ya kiisalaam, Uislaam hutoa majibu ya uadui huo kwa kiwango kidogo iwezekanavyo na kukomea kwenye mipaka yake (na si kuvuka mipaka katika kujibu mashambulizi).

SWALI: Uislaam unahifadhi vipi Amani na Usalama serikalini na kati ya watu?

JAWABU: Hakika utawala au serikali ya-kiisalaam-ni serikali ya wananchi kwa maana sahihi ya neno hilo, watu au wananchi wanataka nini tofauti na kushiriki katika kuchangia rai serikalini, na utajiri, Elimu, Uhuru, Amani, Afya, na fadhila za kimaadili, vitu ambavyo Uislaam unafanya kila mbinu kuhakikisha vitu hivyo vinawafikia wananchi na vinakuwepo tena kwa njia iliyo bora? Na kutokana na sababu hiyo ndio maana tunaona ya kuwa serikali sahihi na utawala safi katika Uislaam ulikuwa ukidumu kwa muda mrefu sana na hilo lilitokana na mapenzi yaliyo kuwepo kati ya wanacnhi na serikali au utawala wao  na Raisi (kiongozi wa juu serikalini) hakuna siku yoyote ambayo alikuwa akihitajia  (Amani) (Ulinzi) (upelelezi) na mfano wa hayo, mpaka ahitaji watu wa kumlinda  na kumuwekea watu wa kumuhami kutokana na watu.

 

UISLAAM NA FAMILIA 

SWALI: Ni upi mtazamo wa kiisalaam kuhusiana na Familia?

JAWABU: Mtazamo wa Uislaam kuhusiana na familia-baada ya kumuangalia mtu mmoja mmoja-ni kuwa familia ndio msingi wa kwanza au tofali la kwanza la msingi katika kujenga jemii njema kwa hivyo Uislaam unakwenda mbio kuhakikisha familia zina kuwa ni familia njema ili jamii iwe njema na nzuri (kwani usafi wa familia ndio sababu ya usafi wa jamii) na kutokana na manti hii tunaona kuwa Uislaam unafaradhisha (kuvaa hijab) kwa mwanamke, Mwenyezi Mungu amesema:

وإذا سألتموهنّ متاعا فاسألوهنّ من ورآء حجاب [30]

(Na mnapo wauliza au mnapo waomba mahitaji basi waombeni kwa nyuma ya pazia)1 na kwa kufanya hivyo matatizo na mabalaa yanapungua na mahusiano ya mume na mkewe  na mke na mumewe yanashika kasi na kuimarika, na hapo familia inakuwa na utulivu na kuishi kwenye anga tulivu na safi, familia yenye kugubikwa na mapenzi na maelewano na utulivu, ikijua ya kuwa Hijab ni: Mwanamke kuto dhihirisha nywele na viungo vyenye kusababisha fitina.

SWALI: Je Uislaam unaharamisha kwa  mwanamke kujielimisha na kufanya kazi?

JAWABU: Hapana, hakika Uislaam haukuharamisha kamwe kwa mwanamke kujielimsha na kufanya kazi, bali Uislaam wakati mwingine umefaradhisha kwa mwanamke kujielimisha  na kufanya kazi na kuvifanya kuwa suna au kuvihimiza kwake wakati mwingine, isipokuwa ilicho kiharamisha Uislaam ni utokaji usio wa kisheria katika nyumba kutojipamba na kujifukizia manukato na na kuonyesha au kudhihirisha mapambo kwa watu wa nje na kuto jisitiri (yaani kutembea bila sitara ya kisheria) kama ambavyo umeharamisha kwa mwanamke kufanya matendo yanayo pingana na sitara yake (iffa) na heba yake. 

 

RAI YA UISLAAM KUHUSIANA NA MWANAMKE

SWALI: Ni ipi rai au mtazamo wa Uislaam kuhusiana na mwanamke?

JAWABU: Uislaam ni Dini yenye huruma sana na hii ni itikadi ambayo imefahamika kwayo Uislaam katika historian na kuitekeleza katika sehemu mbali mbali, ama kuhusiana na mwanamke Uislaam unaona kuwa maisha ya familia hayatimii na kukamilika isipokuwa kwa kuhangaika na kutaabika nje ya nyumba na kuhangaika kwa ajili ya makazi na kufanya kazi ndani ya nyumba, na hapo Uislaam ukagawanya majukumu ya maisha kati ya wawili wenye kuoana kutokana na misingi ya mapenzi na kusaidizana kati yao, mwanamume: ikampatia majukumu ya nje ya nyumba na mwanamke: ukampatia majukumu ya ndani ya nyumba.

Bali kazi za ndani ya nyumba  na utulivu wa ndani ya nyumba majukumu hayo iliyafanya kuwa ni ya mwanamke, kwani mwanamke ndie bora zaidi kuliko mwanamume katika kuendesha mambo ya ndani ya nyumba na hasa katika masuala ya malezi ya watoto kuwalea malezi yaliyo mema na yenye manufaa, mwanamke ni mahala bora kabisa pa malezi na uangalizi na ukuzaji wa kimwili na kiakili na mwenye upole kwa watoto, na Uislaam wenye kusifika kwa sifa ya hekima, umeona ya kuwa lau kama mwanamke ange chukua jukumu la kufanya kazi za mwanamume nje ya nyumba, wakati huo hapana budi azitelekeze kazi zake za nyumbani kwa wanaume na katika kufanya hivyo kuna upoteaji wa nguvu mbili, nguvu ya mwanamke ya huruma na nguvu ya mwanamume ya kufanya kazi, kazi ni ile ile, isipokuwa ni kuwa imegeuzwa na kupinduliwa na hali ikiwa hivyo, katika hali kama hii kwa hakika kutajitokeza au kutatokea natija isiyo ridhiwa wala kuridhisha, kwa hivyo ikapendekeza kuwa mwanamke afanye kazi za ndani ya nyumba na mwanamume ikampatia jukumu la kazi za nje ya nyumba na ambazo ni ngumu.[31] 

  

NDOA KATIKA MTAZAMO WA KIISALAAM

SWALI: Ni ipi rai au mtazamo wa kiisalaam kuhusiana na ndoa?

JAWABU: Uislaam unaona kwamba inajuzu na inafaa kuoa na inatilia mkazo na kusisitiza kufanya hivyo na ina amrisha kuoa na inahimiza kupendekeza jambo la kuoa mapema na uoaji huo ufanyike wakati kila mmoja kati ya mwanamke na mwanamume wamekamilisha miaka ifuatayo, Mwanamke kutimiza miaka tisa (9) pamoja na kufikia ukubwa (kiasi kwamba anakuwa na uwezo wa kuendesha mambo yake) na mwanamume kukamilisha miaka kumi na tano (15), pamoja na kuwa na uwezo wa kuendesha mambo yake pia, na unapo fika wakati huo Uislaam  unatilia mkazo kuoa, ili maovu na ufisadi usiweze kutokea.

SWALI: Ni upi mtazamo wa kiisalaam kuhusiana na mchanganyiko wa mabinti na wavulana (yaani watoto wa kike na kiume), katika tabaka tofauti za uhai wao?

JAWABU: Mchanganyiko wa mabinti na wavulana kwa mtazamo wa kiisalaam-Uislaam ambao unatilia hima kubwa juu ya usalawa wa jamii na saada ya jamii-mchanganyiko huo haufai kamwe, sawa iwe sehemu za kuogelea, mashuleni, au kwenye sinema, au sehemu za kazi, au kwenye mikusanyiko mbalimbali, au kwenye makongamano, au kwenye sehemu zingine, na Uislaam unaona kuwa mchanganyiko huo unasabaisha ufisadi, wakati ambapo ni wajibu kuilinda jamii na ufisadi huo, isipokuwa utakapokuwa mchanganyiko huo una usalama kamili na ulinzi makini na huku kukiwa na hijabu, itara na kutokuwepo uwezekano wa kutokea maovu kwa kuchanganyika kwao kama kuchanganyika katika hijja na sehemu takatifu na mfano wa hizo.

SWALI: Kwa mtazamo wa kiislaam ni yapi majukumu ya mke na mume katika maisha ya kifamilia?

JAWABU:Kwa mtazamo wa kiislaam ni juu ya mume suala la matumizi yote ya mwanamke na kumtosheleza mwanamke matakwa yake ya kimwili-kama ilivyo pangwa katika sheria-na ni juu ya mke kumtii mumewe katika suala la kutoka nyumbani na katika kustarehe, ama mambo ya ndani ya  nyumba si wajibu juu ya mke bali Uislaam unapendekeza kwa mwanamke kufanya hivyo, kwa ajili ya kulinda hali ya kusaidiana na mapenzi kati yao wawili, kisha ni kwamba Uislaam umeifanya nikah (Ndoa) kuwa haifungiki isipokuwa kwa maridhio ya wote wawili  na-Umeiweka talaka-kwa ajili ya maslaha ya kijamii-kuwa ni haki ya mume pekee, isipokuwa ikiwa katika kufunga ndoa watawekeana sharti kuwa talaka iwe ni haki ya mwanamke pia.

SWALI: Ni ipi rai ya Uislaam kuhusiana na kuoa wanawake zaidi ya mmoja?

JAWABU: Uislaam unaona kuwa inajuzu na inafaa kuoa wanawake zaidi ya mmoja hadi kufikia wanawake wane kwa ndoa ya daima lakini kwa sharti kuwa kuwe na ufanyike uadilifu kati yao  na kwa hukumu hii Uislaam ukawa umetatua tatizo la wanawake wasio olewa na wajane, kwa sababu imekuwa maarufu katika jamii mbali mabli na ni jambo lenye kufanyika pia na limethibiti  kwa kufanya sensa kuwa wanawake ni wengi zaidi kuliko wanaume, kwa hivyo basi ikiwa hakukuwekwa ufumbuzi wa kiwango kilicho zidi itakuwa maana yake ni kwamba wanawake wengi watabakia bila kuolewa na bila ya waume.


[1]-Bali matokeo ya maneno hayo ni kuwa: Nidhamu ya utawala wa kiislaam ni bora zaidi kuliko utawala wowote  ulio wahi kutokea na kujulikana katika historia.

[2]- Kwa ajili ya ufafanuzi zaidi rejea kitabu: Min mawsuuatul- fiqhil-kitab (Assiyaasah) siasa na (Al-iqtiswaad) uchumi (Al-ijtimaau) jamii na (Al-idaratu) idara (uendeshaji wa mambo) (Al-hukumu) utawala katika uislaam, na (Al-hurriyatu) uhuru, na kitabu (Idha qaamal islaam fil-iraq) na (Sabilun ilaa inhaadhil muslimiin) na ( As-swiyaaghatul jadiidah) na (Mumaarasatu-taghyiir) na….. cha marehemu Ayatullahil udhmaa Sayyid Mohammad Shiraziy (Mwenyezi Mungu autakase utajo wake).

[3] Al-kafiy: Mujallad wa 2/17.

[4] Suratu twaha aya 125.

[5] Kama ambavyo hakuna shaka juu ya kuwepo kwa vyama au vikundi ambavyo vinafana kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya ujenzi wa nchi ikiwa havipingi kuwepo kwa sheria.

[6] Yaani haki za kisheria, kama Khumsi na Zaka.

[7] Hili kwa sharti kwamba zisivunjwe wala kupuuzwa haki za watu wengine na miongoni mwao ni vizazi vijavyo.

[8] Hakika magazeti na mawakala wa habari wametaja ya kuwa nchi moja wapo kati ya nchi za magharibi yenye nafasi na nguvu katika nchimza magharibi kabla ya miaka kadhaa iliyo pita ilikuwa na tatizo kubwa na uhaba mkubwa wa pesa ya bajeti ya serikali kiasi kwamba inakadiriwa ya kuwa ilikuwa na upungufu wa maelfu kadhaa ya mamilioni ya dola, lakini nchi hiyo iliweza kuziba pengo hilo la bajeti kwa kutumia njia ya kupunguza watumishi wa serikali kwa muda mchache ikaweza kutatua tatizo hilo kubwa na kujilimbikizia hazina kubwa ya ziada inayo kadiriwa kiasi cha mamilioni elfu kadhaa ya dola na kuziweka akiba kwa ajili ya kuinua uchumi wake na hali maisha ya wananchi wake na ni jambo la lisilo fichika ya kuwa, kuwa na watumishi wachache ni jambo lililo amrishwa na uislaam na ni jambo lililo faradhishwa kwa dola la kiislaam, na ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba waislaam wana acha mafunzo ya uislaam wao na wasio waislam kuyatumia mafunzo hayo na wao kupata maendeleo na kutawala na sisi kudhalilika na kubakia nyuma kimaendeleo.

[9] Kama makubaliano ya kisheria au sharti lililo ndani ya makubaliano au mfano wa hayo.

[10] Kipande hiki ambacho kina anwani ya: (Dhamana ya kijamii) kimechukuliwa pamoja na kufanya marekebisho kadhaa kutoka kwenye kitabu: Assiyaasatu min waaqiul- islaam. Cha Mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa Al-haji Sayyid Swaadiq Shiraziy (Mwenyezi Mungu amhifadhi) na kitabu hicho kimechapishwa Iraq mwaka 1381 hijiria, na msambazaji. 

[11] Tafsiru Nuuru thaqalayni: Mujallad wa 4/ 240 na Adhiyaau na Al-aailatu.

[12] Wasailush-shia: Mujallad wa 13/ 151, akinukuu kutoka kwenye kitabu Al-khilaaf.

[13] - Mustadrakul-wasaail: Mujallad wa 2/ 490.

[14] Mustadrakul-wasaail: Mujallad wa 4/ 490.

[15] Mustadrakul-wasaail: Mujallad wa 4/ 492.

[16] Wasailush-shia: kukiwa na marekebisho kadhaa.

[17] Buharul-anwaar: Mujallad wa 32/ 214, kutoka kwa katika kitabu Al-kafiy: Mujallad wa 7/ 354, Mustadrakul- wasaail: Mujallad wa 17/ 446.

[18] Manlaa yahdhuruhul faqiih: Mujallad wa 4/100.

[19] na uchambuzi wa hayo linabakia ni jukumu la bunge la wanazuoni au jopo na shura ya maulamaa na mafaqihi na maraajiu.

[20] Na hili halipingani na kuyapanga hayo, bali makusudio ni kuwa inapsa kuwafundisha wote wakubwa kwa wadogo.

[21] Kama ambavyo inalazimika kuwazuia watu kutengeneza na kupanua uwezo wa makombora au mabomu ya nyukilia ambayo yanamadhara kwa wanadamu na watu wote, kwani ( Hakuna madhara wala kudhuriana katika uislaam) Wasailush-shia: Mujallad wa 17/ 376, mlango wa 1-h 11.

[22] Suratul-anfaal aya 60.

[23]- Suratul baqarah aya 208.

[24] Suratul anfaal aya 61.

[25] Tahdhiibul-ahkaam: Mujallad wa 7/52, hadithi ya 22. Na rejea Wasailush-shia: Mujallad wa 17/ 328, hadithi ya 32228.

[26] Rejea kitabu ( Idha qaamal-islaam fil-iraq) cha Marehemu Ayatullahail-udhmaa Sayyid Mphamma Shiraziy (Mwenyezi Mungu autakase utajo wake).

[27] Na kabla ya miaka khamsini (50) au chini ya miaka hiyo, mambo yote hayo yalikuwa yakitekelezwa kwenye nyumba ya mwanazuoni mmoja wa kiislaam na kulikuwa na karatasi ya kwango cha chini na ya kawaida iliyo kuwa ikitumika kuandikia na kupigwa muhuri wa mwanazuoni yule na mambo ya kibiashara na muamala kati ya watu ukifanyika kwa kutumia karatasi hiyo na wakati huo kulikuwa na usalama na amani na hakukuwa na uzuaji wa karatasi za bandia kiasi kwamba uaminifu uaminifu na amani hiyo iliyo kuwepo inashangaza .

[28]-Suratul baqarah aya 208.

[29] Suratul-anfaal aya 61.

[30] Suratul-ahzaab aya 53.

[31]- Hata kama haikuharamishwa kwake kazi za nje ya nyumba kwa kuzingatia masharti yake.