KUZIENZI NA KUZITUKUZA SHIARI ZA FATIMA

MUHADHARA WA MHESHIMIWA KIONGOZI WA JUU WA KIDINI AYATULLAHIL-UDHMAA SAYYID SWADIQ HUSAINIY SHIRAZIY


(Mungu amzidishie umri).
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu
Amesema mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): Fatuma ni hurul-aini wa kibinadamu, kila nilipokuwa na shauku ya kunusa harufu ya peponi basi hunusa harufu ya binti yangu Fatuma. (Al-amaaliy cha Swaduuq hadithi namba 546).
Sifa zote njema zinamstahiki Mola wa viumbe wote na rehma na amani ziwe juu ya Muhammmad na Aali zake wema na watwaharifu, na laana iwe juu ya maadui zao wote daima na daima.

 

FATIMA (A.S) NDIE MSINGI WA AHLUL-BAITI

Katika hadithi ya kisaa (Shuka) ambayo ni hadithil qudsi iliyo pokelewa kutoka kwa Sayyidatina Fatima Zahraa (a.s) imepokelewa kuwa Jibrilu alimuuliza Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kusema: Ni akina nani hao walioko chini ya kisaa? Na Mwenyezi Mungu alipo taka kuwataarifisha na kuwatambulisha wale watu watano wema na watwaharifu akasema: Wao ni Fatima na baba yake na mumewe na wanawe.
Huenda utambulishaji wa aina hii ni utambulishaji wa aina ya pekee kati ya mifumo ya Mwenyezi Mungu ya kumtambulisha mtu au kitu, kwani ni jambo lisilo na shaka kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) ni bora kuliko Fatima, na haya ndio tuyaonayo hata katika kubainisha mambo ya kisheria ya wajibu na sunna, kwa mfano katika Tashahudi ya sala ya wajibu tunaanza tashahudi hiyo kwa kumsalia Mtume (s.a.w) kisha wanafuatia Aali zake (a.s).
Kwani twatambua kuwa kanuni halisi katika kukitambulisha kitu ni kuwa unaaanza kwa kutaja kilicho bora na kilicho wazi kabisa au chenye kujulikana sana, lakini sisi katika hadithil hii qudsi tunaona ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amebadilisha mfumo huo katika kuwatambulisha watu hawa, kwani amemfanya Fatima (a.s) kuwa ndio msingi wa utambulisho, wakati ambapo ilikuwa ni lazima- kidhahiri –kuanza kumtambulisha Mtume (s.a.w.) kisha Ahlil-baiti wake (a.s).
Na swali hapa ni kama lifuatalo: Je malaika hawakuwa wakimfahamu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) kabla ya utambulisho huo? Bila shaka yoyote walikuwa wakimfahamu Mtume wa Mwenyezi Mungu na wakimfahamu Amiril-muuminiin na Husein (a.s) isipouwa ni kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu aliwataarifisha kupitia kwa Fatima Zahraa (a.s), sasa kitendo hiki kinajulisha nini au kinatoa dalili gani?
Jawabu: Kitendo hicho kinatujulisha na kututambulisha juu ya nafasi ya juu ya bibi huyo (a.s), na Mwenyezi Mungu mtakasifu na mtukufu ameashiria sehemu ndogo tu ya nafasi hiyo katika maneno haya machache, kwani amesema:

( فاطمة وأبوها وبعلها وبنوها) (Fatima na baba yake na mumewe na na wanawe).
Sisi hivi sasa tuko ukingoni mwa masiku ya Fatima (a.s), na kwamba Swiddiqah Zahraa (a.s) kutokana na aliyo yastahmili na kuyavumilia kwa hiari yake na kukubali kwake kuivumilia misiba mizito na mikubwa, Mwenyezi Mungu akamchagulia nafasi ya juu ambapo ameielezea sehemu ndogo tu ya nafasi hiyo katika neno hili, kwani alimtambulisha Mtume (s.a.w) kupitia kwa pande lake la nyama ambalo ni Swiddiqatuz-zahraa alie mtwaharifu (a.s).
Ni wakati gani imeonekana na kutokea katika historia ya kuwa alie bora hutaarifishwa na kutambulishwa na alie kuwa chini yake (yaani asie bora kuliko yeye)? Na ni wakati gani kitendo kama hicho kilitokea kabla ya kutokea kwa Swaidiiqah Zahraa (a.s)? hakuna shaka kuwa Swaiddiqah Zahraa yuko katika njia ile ile na mwenendo uleule wa baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) isipokuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutumia kwake mfumo huu alitaka kubainisha nafasi na maqaam ya Fatima (a.s)?!