2- UADILIFU WA ALLAH

Maana yake ni kuwa: Mwenyezi mungu ni muadilifu hamdhulumu yeyote na hafanyi mambo yaliyo kinyume na hekima, kwa hivyo uumbaji wote, na utoaji wa riziki, utoaji na uzuiaji, vyote hivyo vimefanyika kutokana na maslahi au hufanyika kwa maslahi hata kama hatuyajui maslahi hayo, kama ambavyo Daktari anapo mtibu mtu fulani kwa kumpatia dawa fulani hufahamu ya kuwa dawa hiyo inamanufaa hata kama hatukufahamu maslahi yenyewe yaliyomo kwenye dawa hiyo.

Kwa hivyo basi tutakapo ona ya kuwa Mwenyezi Mungu amemtajirisha mtu fulani au mtu fulani amemtia ufukara, au mtu fulani amemfanya kuwa mtukufu (sharifu) na mwingine hakumfanya hivyo, au amemtia ogonjwa mtu fulani na hakumfanya mtu mwingine kuwa mgonjwa, na mfano wa hayo, nilazima kuitakidi ya kuwa yote hayo yamefanyika kutokana na maslahi na hekima hata kama hatufahamu hekima yake na maslahi yake.[1]

Na imepokelewa katika hadithi: Yakuwa Mussa (a.s) alimuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amfahamishe na kumtambulisha sehemu fulani ua uadilifu wake-kati ya mambo ambayo dhahiri yake ni mushkeli (ni tatizo kuyaelewa), Mwenyezi Mungu akamuamrisha aende kwenye kisima chenye chemchem jangwan, ili akaangalie ni kitu gani kitafanyika huko,  pindi Mussa (a.s) alipo toka alimuona mpanda farasi akija na kufika kwenye kisima hicho na kutelemka kutoka juu ya farasi wake na kukidhi mahitaji yake sehemu hiyo, na baada ya kumaliza alianza safari na kuondoka na kusahau mfuko wake wa pesa sehemu hiyo, kisha baada ya muda fulani akaja mtoto mdogo aliekuwa mumayyizi (yaani mwenye kutambua mambo) mtoto yule aliuona mfuko ule ukiwa umedondoka chini pembezoni mwa kisima kile, akauokota kwa furaha kubwa na kuondoka kwa haraka kurejea aliko toka, kisha baada ya muda akaja kipofu kwa ajili ya kutawadha kwenye kisima kile, ghafla yule mpanda farasi akarudi na kufika mahala pale huku akitafuta mfuko wake wa pesa, baada ya kuutafuta na kutouona akamtuhumu yule kipofu ya kuwa ndie alie chukua na kukapita mvutano kati yao, mvutano ulio pelekea yule bwana kumuua kipofu na yule mpanda farasi kujificha na hapo Mussa akastaajabu kutokana na yale aliyo yaona na kushangaa sana, Mwenyezi Mungu mtukufu akamtelemshia wahyi kwa mambo yaliyo ondoa mshangao wake, kwani alimwambia: Mpanda farasi alikuwa ameiba mali ya baba wa yule mtoto, kwa hiyo ile mali tukairudisha kwa mrithi  ambae ni yule mtoto ambae umemuona, na yule kipofu alikuwa ni muuaji wa baba wa mpanda farasi, kwa hiyo mrithi akachukua haki yake na kulipiza kisasi kwa kipofu yule.[2]

Na hivyo ndivyo hukumu ya Mwenyezi Mungu inavyo kuwa na uadilifu wake japokuwa kwa mtazamo wa juu juu jambo hilo liko mbali na kanuni. 


[1] -  Pamoja na haya ukiongezea mambo mengine mengi yaliyo tajwa kama ufukara Magonjwa na mfano wa hayo yanatokana na matumizi mabaya ya mwanadamu mwenyewe na kuto pangilia vema au kuto weak mipango mizuri. Zinhatia katika hilo.

[2] - Buharul-anwaar: juzu ya 61/ 117 malango wa 2/ chapa ya Bairut.