MAREJEO YA KIAMA 

Maana yake ni kuwa: Mwenyezi Mungu mtukufu anamuhuisha na kumfanya mwanadamu awe hai katika Akhera baada ya kumfisha duniani, ili amlipe thawabu mtu mwema juu ya wema wake na kumlipa muovu kwa uovu alio ufanya.

Kwa hivyo basi mwenye kuamini na kutenda matendo mema na kusali, kufunga, katoa sadaka (zaka) na kumtakasia nia Mwenyezi Mungu (kuwa na ikhals) na kuwahifadhi Mayatima na kuwalisha Masikini na mengineyo mengi, hakika yeye Mwenyezi Mungu humpa thawabu mtu huyo kwa kumuingiza kwenye pepo yenye neema ambayo hutiririka chinio yake mito, na yenye vivuli vyenye kumfunika na yenye rehma nyingi sana na majumba ya kifalme na kifakhari na mahurulaini walio fungiwa kwenye majumba yao na kupata maridhio ya Mwenyezi Mungu ni kukubwa zaidi.

Na mwenye kukufuru na kufanya matendo mabaya na kusema uongo,  kufanya khiyana, kuua, kuiba, kuzini, kunywa pombe, na mfano wa hayo, hakika Mwenyezi Mungu humlipa kwa kumuingiza katika jahannama iliyo jawa na moto na adhabu, na chakula chake ni cha miti ya miba na kinywaji chake ni maji ya moto na wakati yuko kwenye matatizo na adhabu yenye kudhalilisha na ya milele isio katika wala kukoma.

Na kuna visimamo vingine viwili kabla ya moto na pepo:

1-Kaburi: Nayo ni sehemu au hatua ya kwanza kati ya hatua za ulimwengu wa barzakh baada ya kuwa mauti ni mlango wa kuingia kwenye ulimwengu huo, kwa hivyo kila mmoja huulizwa aliyo yafanya akiwa kaburini mwake, na kupewa thawabu kwa matendo mema aliyo yatenda na kuadhibiwa juu ya matendo mabaya na kutokana na hayo Mtume (s.a.w) akasema: (Kaburi ima ni shimo kati ya mashimo ya moto, au ni bustani kati ya mabustani ya peponi) [1] na hali ya mwanadamu akiwa kaburini kwa mfano na kwa kutaka kukuletea karibu maana na hali yake ni kuwa: ni kama hali ya mtu alie lala ambae anaota ndoto nzuri na kufurahi kwa ndoto hiyo, au kuota ndoto mbaya na kuteseka na kuadhibika kwa ndoto hiyo, wakati ambapo yule ambae humkaribia yule mtu alie lala na kumuona, hafahamu ya kuwa yuko kwenye raha au kwenye adhabu, vilevile walio hai huwaoni watu walio kufa katika hali ya kuwa ni vilivyo haribika, ama kujua ya kuwa wana adhibiwa au wako kwenye neema, hawalihisi hilo na hilo linatokana na ukweli kuwa vipimo katika ulimwengu wa barzakh ni vipimo vipya tofauti na vipimo vya duniani, na havifanani na vipimo vya maisha ya kidunia ambavyo tunavifahamu na tumevizowea.

2-Kiama: Nayo ni kuwa baada ya kuvifufua viwiwili hivi na kuvitoa kwenye makaburi, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu atavifufua katika siku hiyo vyote katika jangwa kubwa na pana kwa ajili ya hesabu na malipo na huko kuwekwa mahakama kubwa na kuwekwa vipimo na mahakimu kuhudhuria-nao ni mitume wa Mwenyezi Mungu na mawasii wao-na kugawiwa madaftari ya matendo: Nyaraka za matendo ya waja na mashahidi kwa ajili ya kutoa ushahidi, na viungo vya mwanadamu kukiri juu ya matendo yaliyo tendwa na mwanadamu na kuyafanya, na waumini wale ambao walifanya matendo mema duniani kuneemeka kwa kuingia peponi na waovu wale ambao walikuwa wakitenda maovu duniani  kuwa katika hali mbaya ya uovu na kuingia motoni. 

Kwa hivyo ni juu ya mwanadamu kujitahidi kwa kadri ya uwezo wake katika kutekeleza matendo mema na kujiepusha na matendo maovu, ili asije kuwa muovu huko katika Akhera uovu wa milele na milele, uovu usio kuwa na makimbilio wala muokozi, kiasi kwamba waovu watabakia jela wakati wote na wakiwa kwenye adhabu ya milelel.

Mwenyeziu Mungu anasema:

(فمن يعمل مثقال ذ رة خيرا يره.  ومن يعمل مثقال ذ رة  شرا يره) [2]

Mwenye kufanya matendo ya kheri hata kama ni kiasi cha tembe moja atayaona. Na mwenye kufanmya matendo ya shari kiasi cha tembe moja atayaona.


[1] - Rejea kwenye kitabu  Al-aamaaly cha Shekh Mufiid, ukurasa 265, majlis ya thalathini na moja (31).

[2]- Suratuz-zilzaalah aya 7-8.